ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 9, 2011

TANZANIA INVESTMENT FORUM 2011

Wizara ya Nishati na Madini ikishirikiana na ubalozi wa Tanzania Uk wameandaa kongamano la uwekezaji nchini. Hii ni katika kutekeleza sera za economic diplomacy pamoja na kuvutia mitaji ya kigeni. Mh Ngeleja.
Mada nyingi zilizungumziwa kuhusu nafasi na sheria za uwekezaji Tanzania ambapo Waziri Ngeleja kama mgeni rasmi na mwakilishi wa taifa aliwaweka wazi wawekezaji jinsi ya sheria mpya zilizotungwa na kuwahakikishia kuwa Tanzania na Watanzania wako tayari kupokea wawekezaji ambao wako tayari kuwekeza ilimradi waje na njia ambazo hazitinyinya Watanzania na taifa lao.
Dr Abdelhelm Meru Mkurugenzi mkuu wa EPZA akitoa mada iliyosisimua kuliko zote

Balozi Peter Kallaghe akitafakari.
Eneo lililovutia sana washiriki lilikuwa eneo la nishati na madini pamoja na viwanda. Waekezaji ambao tayari wako nyumbani Tanzania wametoa sifa kwamba kwa sasa Tanzania inawezekana kuwa ndio nchi pekee Afrika yenye mazingira sawia kwa wawekezaji toka nje.
Mh ngeleja akibadilishana mawazo na Naibu Balozi chabaka na Moja ya wanakongamano

Waziri Ngeleja akiwa na Wajumbe wa JumuiyaTanzanian Uk
Mwanataaluma bi Barbara Njau alifafanua kwa ushahidi wa vielelezo kuwa uchumi Watanzania siku zijazo utakuwa haraka sana na kuwa Watanzania na nchi yao kwa ujumla kwa ujumla wako kwenye nafasi nzuri kabisa kimaendeleo kama watatumia rasilimali walizonazo kwa umakini na uangalifu.
Chanzo:Urban Pulse Creative.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.