ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 9, 2011

TAMASHA LA KUWAENZI WAIMBAJI WA RWANDA WALIOFARIKI KUFANYIKA MWANZA JUMAPILI HII

Kwaya ya The Ambasador of Christ kutoka Kigali nchini Rwanda imewasili jijini Mwanza kwaajili ya tamasha la Kuimba na kushukuru linalotegemewa kufanyika siku ya jumapili jijini hapa.

The Ambasador of Christ wamewasili salama salmini.

Mmoja kati ya majeruhi wa ajali kwaya ya The Ambasador akisalimiana na wanakwaya wawakilishi Mwanza.

Salaam salaam...!!

The Ambasador wakisalimiana na kwaya wenyeji jijini Mwanza.

Kwaya wageni kutoka nchini Rwanda ya The Ambasadors of Christ almaarufu kwa jina la 'Kwetu Pazuri' imeshuka jijini Mwanza kutuliza kiu ya burudani ya muziki wa Injili kupitia zinduzi za album zake tano kwa mpigo ikiwemo singo 'kwetu pazuri' iliyo watambulisha na kuvuma kote Afrika Mashariki.

Lengo kuu la Tamasha hilo ni kutoa shukurani kwa watanzania kwa moyo wao wa upendo waliouonyesha kwao kuwasaidia pindi walipopata ajali iliyotokea mwaka jana hapa nchini huko wilayani Kahama na kundi hilo kupoteza waimbaji wake watatu.

Sehemu ya waimbaji kwaya ya The Ambasador of Christ.

Usikose siku ya jumapili ya tarehe 11mwezi huu katika dimba la CCM Kirumba, jijini Mwanza ambapo tutakutanishwa kwenye kusanyiko kubwa la Tamasha la muziki wa Injili lililo chini ya usimamizi wa Maua Music Centre ambapo kwaya na makundi mbalimbali kukusanyika na kutoa burudani ya nyimbo za sifa.VIDEO - 'Kwetu pazuri'

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Karibuni sana ndugu zetu, nawafagilia kinoma kwa uimbaji wenu.

    ReplyDelete
  2. ambasadors barikiwa,nimeipenda huduma yenu pia nabariwa na uimbaji wenu.ni vipi naweza kuwasiliana nanyi,

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.