ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 6, 2016

MUME AMUUWA MKE WAKE PAMOJA NA MTOTO KWA KUWACHINJA NA KISU WILAYANI BAGAMOYO MKOA WA PWANI

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO

JESHI la polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Frowin Mbale (26) ambaye ni mkazi wa kawe Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kufanya mauaji ya kikatili ya  mke  pamoja na mtoto  wake kwa kuwachinja  shingoni na kisu kasha kuwatupa vichakani.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Boniventura Mushongi amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kudai kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 10:30 jioni katika kijiji cha zinga  kata ya Dunda Wilayani Bagamoyo.

Kamanda Mushongi amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na mwenzake  mmoja  aliyejulikana kwa jina la Rajabu Juma (20) na walifanikiwa kuwakamata juzi usiku majira ya saa 2:30 katika maeneo ya  kijiji cha zinga.

Pia Kamanda Mushongi amewataja marehemu hao kuwa ni Oliver Erasto (200 pamoja na mwanae Emmanuel Frowin (3) ambao miili yao ilikutwa imetupwa katika vichaka vya kaole kata ya dunda

 “Kutokana na tukio hili watuhumiwa wote kwa sasa tumewashikiria baada ya kutaka kutoroka ila kwa bahati nzuri wananchi waliweza kutoa taarifa mapema kwa vyombo vinavyohusika na ndipo walipofanikiwa kuwakamata,”aisema Kamanda Mushongi.

Aidha alifafafnua kuwa mtuhumiwa huyo akiwa na rafiki yake walimlaghai mkewe waongozane pamoja wakiwa na mototo wao kwenda kuangalia ujenzi wa nyumba yao unaoendelea katika eneo la kaole lakini walipofika huko ndipo walipoamua kufanya tukio la mauaji hayo ya kikatili.

Mushongi akielezea zaidi kuhusiana na tukio hilo amesema uchunguzi walioufanya umebaini mauji hayo yametokana  na wivu wa mapenzi, ambapo mume  huyo alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano wa kimapenzi na mtu mwingine aliyejulikaana na kwa jina la moja la Hamza mkazi wa kawe.

Katika hatua nyingine Mushongi amelaani vikali tabia kama hiyo na kuwataka wazazi na walezi Mkoani Pwani kutovunja sheria kwa kujichukulia sheria mikononi kwani  kufanya hivyo ni kinyume cha taratibu na sheri za nchi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.