ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 7, 2016

FNB SASA RASMI JIJINI MWANZA.

 Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema mkoa wa Mwanza una uwezo mkubwa wa kiuchumi na ukuaji mkubwa wa sekta mbalimbali za kiuchumii karibuni ni ishara kuwa Mwanza inakua kwa kasi.

"Tunakaribisha uwepo wa FNB  na tunatazamia kuwasaidia kuimarisha huduma zenu hapa na  mikoa mengine," alisema Mkuu wa Mkoa.

Alisema mbali na mkoa wa Mwanza kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi bali pia inazalisha mali nyingi na ina utajiri mkubwa wa rasilimali. 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya FNB Tanzania la Mwanza jana jijini humo huku akiambatana na Mkuu wa Biashara wa FNB Tanzania, Francois Botha (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma (kulia) na Alex Mziray, Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo.
 “Tunatarajia kuwa mtatoa mchango mkubwa katika utoaji huduma za kifedha mkoani Mwanza kupitia huduma zenu mbalimbali kwa kutumia ubunifu na utaalamu wenu,” Mongella alisema.
Wadau wa kibiashara na wawekezaji.
 First National Bank ni benki inayotoa huduma kwenye nchi mbalimbali barani Afrika tangu mwaka 1874.
Hivi sasa FNB inatoa huduma zake kwenye nchi za Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Zambia, Mozambique, Lesotho, Swaziland na Tanzania na mpango wake ni kuwa benki inayohudumia watu wengi zaidi barani Afrika.



 Benki ya First National Bank Tanzania (FNB) imeendelea kupanua wigo kitaifa kwa kufungua tawi jipya eneo la Rock City Mall jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akisalimiana na mmoja kati ya wadau wa FNB baada ya kutinga ndani ya Benki hiyo kama sehemu ya ufunguzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma akisalimiana na mmoja kati ya wadau wa FNB baada ya kutinga ndani ya Benki hiyo kama sehemu ya ufunguzi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akipata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na benki ya FNB Tanzania kutoka kwa Asmini Gambo, Mshauri wa Huduma kwa Wateja na Mauzo wa benki hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua huduma za benki hiyo jijini Mwanza.
 Mkuu wa Biashara wa FNB Tanzania, Francois Botha akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma (kulia)  jinsi ya kuhamisha fedha na kupata huduma za kifedha kupitia simu ya mkononi. 
 Mkuu wa Biashara wa FNB Tanzania, Francois Botha akimueleza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella jinsi mashine ya kisasa ya kutolea fedha inavyofanya kazi baada ya mkuu huyo wa mkoa kuzindua huduma za benki hyo jijini Mwanza.  Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akizungumza na waandishi wa habari.
Yapi manufaa kwa ujio wa FNB.
Mkurugenzi Mkuu wa Nyanza Bottling, Christopher Gachuma alifunguka jinsi jamii itakavyoufaika na shughuli za kibenki.
Pamoja sana.
Sehemu ya kusanyiko la uzinduzi.
Uzinduzi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mkuu wa Biashara wa benki hiyo, Francois Botha alisema uzinduzi wa tawi la FNB Mwanza umelenga kukidhi ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma za kibenki na za kifedha katika mkoa huo.

  “Uzinduzi wa tawi la Mwanza ni sehemu ya uwekezaji endelevu na mkakati wa kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanapata huduma bora za kifedha. Pia tumezingatia ukuaji wa haraka wa mkoa wa Mwanzaambao una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania.”

Botha alisema tawi Mwanza ni la tisa miongoni mwa mtandao wa matawi ya FNB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati  wa kupanua mtandao wa matawi ili kuyafikia maeneo yote nchini.

“ First National Bank daima tunafikiri njia mbalimbali za  ambazo tunaweza kutoa huduma za kibenki kwa urahisi kwa wateja wetu. Tawi letu la  Mwanza litatoa ufumbuzi wa kina kwa wateja wanao ishi Mwanza na maeneo jirani  yenye biashara inayokua kwa kasi” Botha alisema.

Mara kwa mara tunafikiria mbinu mpya za kutuwezesha kutoa huduma inayowapa unafuu wateja wetu kwa kupeleka huduma hiyo karibu na makazi pamoja na biashara zao. Tawi hili litarahisisha huduma kwa wateja wetu wanaoishi jijini Mwanza na maeneo ya jirani ambayo yana biashara nyingi zinazokua kwa kasi,” alisema Botha.
Picha ya pamoja.
G.Sengo.
Tawi hili lililofunguliwa kwenye jingo jipya la Rock City Mall litatoa huduma za kawaida za kibenki pamoja na huduma za dijitali kwa masaa 24 ili mahususi kukidhi mahitaji ya watumiaji huduma pamoja na wafanyabiashara katika eneo hilo.

First National Bank Tanzania ilifungua milango yake rasmi nchini Tanzania tarehe 27 Julai 2011, tawi la Mwanza likiwa ni la tisa, matawi mengine ni pamoja na tawi la makao makuu, Mbezi Beach, Sinza, Mbagala, Quality Centre, Peninsula, Kariakoo na tawi la Kimweri. 

Kwa taarifa zaidi tembelea www.fnbtanzania.co.tz au tuma barua pepe info@fnb.co.tz

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.