Hayo
ni kwa mujibu wa ripoti ya siri ya Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa kwa
Baraza la Usalama la umoja huo na jopo la waangalizi wa vikwazo dhidi
ya nchi hiyo.
Waangalizi
hao wa UN wamesema, asilimia 97 ya mapato yanayotangazwa rasmi ya
serikali ya Sudan Kusini yanatokana na mauzo ya mafuta huku asilimia
isiyopungua 50 ya mapato hayo ikitumika kwa masuala ya usalama.
Jopo
hilo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa limefafanua katika ripoti yake
hiyo kuwa mapato yaliyotokana na mauzo ya mafuta yaliyouzwa kuanzia
mwishoni mwa mwezi Machi hadi Oktoba 2016 yalikuwa karibu dola milioni
243, lakini licha ya ukubwa wa matatizo ya kisiasa na hali mbaya ya
kibinadamu na kiuchumi iliyopo serikali ya Rais Kiir imeendelea kununua
silaha kwa ajili ya jeshi lake la Ukombozi la Wananchi wa Sudan (SPLA),
vikosi vya huduma za usalama wa taifa, vikosi vingine tanzu pamoja na
wanamgambo watiifu kwa serikali hiyo.
Umoja wa Mataifa ulitangaza baadhi ya maeneo ya taifa hilo changa
zaidi duniani kuwa yamekumbwa na baa la njaa ambapo watu wapatao milioni
tano na nusu, ikiwa ni takriban nusu ya raia wote wa nchi hiyo
wanakabiliwa na uhaba wa chakula.
Raia wa Sudan Kusini wanaokabiliwa na ukame. |
Machafuko
na vita vya ndani vilizuka nchini Sudan Kusini Desemba mwaka 2013 baada
ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake, Riek Machar kwamba
amehusika na jaribio la kutaka kupindua serikali yake
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.