ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 29, 2019

MWENYEKITI UVCCM AKEMEA SIASA ZA MAKUNDI

 Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara akemea Siasa za makundi na kudhoofishana

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Mara, Ndg Kheri D. James (MCC) amekemea vikali tabia ya baadhi ya Wanachama cha CCM kuanza kampeni mapema na kuchafuana. 

Ameyasema hayo leo, Alhamis tarehe 28-03-2019  akiwahutubia wajumbe wa halmashauri ya CCM Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara. Ndg Kheri D. James (MCC) alionya kwamba, chama hakitamuhurumia yeyote anayeendesha makundi na siasa za kudhoofishana zinazolenga kuwagawa wanachama na kukosesha ushindi kwenye chaguzi.
Awali akiongea na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Wilaya, Comrade Kheri D. James alieleza juu ya watendaji na viongozi wa CCM kuheshimu katiba na kanuni zingine za Chama. 

Alisisitiza kushirikiana na kupendana huku wakizingatia mgawanyo wa majukumu uliowekwa ili kuepuka migongano isiyokuwa na sababu.

Ndg Kheri D. James alitumia ziara hii kukumbusha viongozi wa ngazi mbalimbali kuwa na mikakati ya kuweza kujitegemea kiuchumi. Alieleza kwamba ni wakati sasa CCM na Jumuiya zote ziweze kujiendesha zenyewe kwenye ngazi za Wilaya.

Amewaomba Viongozi  na wanachama wa CCM kuungana na Rais wetu, Mhe. Dkt. John Joseph Magufuli katika vita dhidi ya Rushwa. Amewataka kukemea vitendo vya Rushwa kwani vinapelekea kuzorota kwa utolewaji wa huduma za kijamii, Ujenzi wa miundo mbinu isiyo na Ubora na pia kupatikana kwa viongozi ambao hawana uwezo kuleta matokeo chanya. Vile vile Rushwa inapelekea kushamiri kwa dhulma,ongezeko la urasimu katika upatikaniji wa haki na fursa.Na wahanga wakubwa wa rushwa ni sisi Vijana.

Comrade Kheri D. James ameanza ziara ya kikazi kama Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara kukagua uhai wa chama kwa kukumbushia taratibu na kanuni zinazoziongoza Chama cha Mapinduzi,kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama na kuweka mikakati kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019. 

Ziara hii itakuwa ni kwa Wilaya za Mkoa wa Mara kwa kuanzia Serengeti, Tarime, Rorya, Musoma Vijijini,Musoma na Bunda.       _Mwisho

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.