Mwakilishi wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu
(Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akikabidhi msaada wa mabati kwa mkuu wa
wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo
Mwakilishi
wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja
na Asmah Abubakar(kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi
msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo (kulia)
Mwakilishi
wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja
na Asmah Abubakar(kushoto) kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi
msaada wa mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo (kulia)
.
Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo, mkuu wa Wilaya ya Kilindi akikabidhi mabati
yaliyotolewa na BancAbc kwa walimu wa shule ambazo zimenufaika na msaada huo.
Mwakilishi
wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akiwa pamoja
na Asmah Abubakar kutoka kitengo cha masoko wa BancABC wakikabidhi msaada wa
mabati kwa mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo
Mwakilishi
wa benki ABC Bw. Emmanuel Nzutu (Mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi) akipeana
mkono na mkuu wa wilaya ya Kilindi Mh. Sauda Mtondoo baada ya kukabidhi msaada
wa mabati 200. Wengine katika picha ni Asmah Abubakar na Raphael Kalinga wa
BancAbc.
BancABC kupitia Huduma yetu ya Mkopo Rahisi imejidhatiti kuweza kuhakikisha kwamba tunainua kuendeleza mazingira ya elimu katika wilaya ambazo benki hii inafanya shughuli zake kupitia miradi yetu ya kusaidia jamii inayotuzunguka.
Sisi BancABC tunaamini kwenye umuhimu wa elimu bora katika jamii zetu hapa Tanzania na kwa hivyo tunaunga mkono Serikali ya Awamu ya 5 na hususani Rais wetu Mhe. John Pombe Mafuguli Katika miradi mbali mbali ya elimu kwa lengo la kuinua kiwango cha elimu na kuweza kuwafikia kila jamii na hasa maeneo ya vijijini kwa wale ambao wako kwenye hali duni.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi Bw. Emmanuel Nzutu ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo rahisi alisema; “Kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure kwa kila Mtanzania kuanzia chekechekea hadi kidato cha nne, Leo Bancabc tunatoa msaada wa mabati 200 kwa wilaya ya Kilindi, na msaada huu tunaukabidhi hapa kwa Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Sauda Salum Mtondoo.”
Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha Bancabc na pia kuwajulisha kuwa benki yetu tunatoa huduma ya Mkopo ambao ni mahususi kwa wafanyakazi wa serikali, Easy loans ambapo inakupa nafasi ya kulipa Mkopo kwa muda wa miaka sita na vile vile una uwezo wa kuweza kuongeza Mkopo hata kabla ya kumaliza kulipa ule wa awali.
Uzuri wa mkopo huu tofauti na mikopo mingine ni kwamba, mwenye kuomba Mkopo anaweza kuchagua ni mradi gani wa kuwekeza fedha zake kwa mfano kulipa karo ya shule, kununua gari, kufanya marekebisho ya nyumba, kulipa kodi ya nyumba au kumalizia ujenzi.
Vile vile tunaweza kununua Mkopo wako wa awali ukabaki na Mkopo mpya.
‘Mkopo huu utakuwa na bima ya maisha pale ambapo mwenye Mkopo anapofariki, familia yake inapewa pesa taslimu Tzs500, 000 kwa ajili ya kugharamia mazishi.’
Tunatoa wito kwa wateja wetu na wale ambao pia sio wateja wetu kujiunga na Bancabc na kuchangamkia Mkopo huu kwani sisi tunakuweka karibu na ndoto zako.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.