ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 19, 2012

MICHUANO YA SITA YA BANDARI TANZANIA YAMALIZIKA LEO JIONI JIJINI MWANZA.

Michuano ya sita ya bandari imemalizika leo jijini Mwanza kwa washiriki mbalimbali kutunukiwa nishani zao, makombe na  zawadi za fedha.


Michuano hiyo kabla ya kufungwa iliambatanishwa na maandamano kwa wawakilishi wa timu zote kutembea umbali mfupi hadi uwanja wa CCM Kirumba hatimaye kupita mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga.

Timu ya Bandani Dar es salaam ikipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi.

Timu ya Bandari Tanga.

Bandari Mtwara.

Bandari za Maziwa. 

Mshindi wa mbio za kufukuza kuku Oliver Ngumuo kutoka Bandari ya Dar es salaam akiwa na zawadi yake.

Timu ya Bandari za Maziwa. 

Timu ya Bandari ya Tanga.

Mashabiki nao hawakuwa nyuma katika kusapoti timu zao.

Katika mchezo wa kuvuta kamba Bandari Tanga (kulia) waliibuka kidedea kwa kuwazidi ubavu timu ya Bandari za Maziwa Makuu (kushoto).

Timu ya Bandari Dar es salaam ndiyo iliyotia fora kwa kunyakuwa vikombe vingi hapa Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kombe la ubingwa kwa timu hiyo upande wa soka.

Timu ya Bandari Dar es salaam ndiyo iliyotia fora kwa kunyakuwa vikombe vingi hapa Mh. Baraka Konisaga akikabidhi kombe la ubingwa kwa timu hiyo upande wa mpira wa pete.



Timu ya Bandari Dar es salaam ndiyo iliyotia fora kwa kunyakuwa vikombe vingi hapa na hapa wakisherehekea tuzo na makombe waliyonyakuwa.

Timu ya pili kwa ushindi wa jumla ni Bandari Tanga.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.