ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 19, 2012

TIGO YAZINDUA MAJUKWAA YA UJASILIAMALI NCHINI

Mwezeshaji wa Jukwaa kutoka Tigo Makao makuu  Hubert Luis  akifungua Jukwaa hilo ndani ya Hoteli ya Gold Crest Mwanza kwa niaba ya Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutirrez.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo leoimezindua majukwaa kwa ajili ya wajasiliamali wapya nchi nzima kama sehemu ya wajibu wake katika kusaidia na kukuza wajasiliamali wadogowadogo na wakati nchini.

Lengo la majukwaa hayo ni kuwaleta pamoja wajasiliamali na mashirika ya kibiashara kutoka sekta mbalimbali ili kupanua mitandao yao na kunufaika na suluhu mpya za mawasiliano kwa biashara. Biashara ndogo na za kati zitanufaika na warsha, mafunzo na mazungumzo ya mada zinazohusu masoko, menejimenti, fedha na uzalishaji.
Ridhiwani Kassimu mtaalamu wa biashara ndogondogo na kati kutoka benki ya NBC akitoa somo.
Pamoja na kufafanuwa kuhusu vifurushi maalum vya kiteknolojia vya mawasiliano, bwana Ridhiwani Kassimu mtaalamu wa biashara ndogondogo na kati alitoa somo kwa wajasiliamali na waendeshaji biashara kupitia mada ya "Jinsi ya kupata mitaji kwa biashara yako"
Hapa wadau walielimishwa madhara ya kuomba mkopo kwa muda mrefu, Ushauri kwa wafanysbiashara kuhusu mikopo, Masuala gani yanawanyima wajasiliamali mikopo, Vihusishi gani vinaisababisha benki kuwa rahisi kutoa mkopo pamoja na Miiko ya mjasiliamali anayopaswa kufuata wakati wa uombaji mkopo.

Mc wa Jukwaa hilo Costantine Magavila akitoa ufafanuzi.

Utambulisho kwa wadau muhimu wa Togo Kanda ya Ziwa.

Huyu ni Injinia wetu...si mtu wa maneno bali vitendo zaidi

Miongoni mwa suluhu bunifu za kibiashara zitakazozinduliwa kwenye majukumu haya ni vifurushi maalum vya kiteknolojia vya mawasiliano, 'Tigo TELCO Solutions', vinavyolenga kuwa sehemu moja pekee yakukidhi mahitaji yote ya mawasiliano ya kibiashara.

Vifurushi hivi vitatoa mbinu za kuwapa wajasiliamali ufanisi kwenye matumizi na kuwawezesha kupanga mipango yao ya kibiashara ndani ya bajeti zao. Pia inawapa wajasiliamali fursa kuwasiliana na wadau kwa unafuu zaidi pamoja na chaguo mbilimbali za kulipia bili.

Wadau mbalimbali wakiendelea kupata vitafunwa huku wakipokea somo kutoka Jukwaa la leo lililofanyika kwenye Hoteli ya Gold Crest mkoani Mwanza.

Jukwaa la leo limefanyika hapa Hoteli Gold Crest mkoani Mwanza. majukwaa mengine yatafanyika kwenye miji mingine Tanzania hadi mwisho wa mwaka hivyo wadau mikoa mingine kaeni tayari twaja.....

Wadau mbalimbali wakiendelea kupata vitafunwa huku wakipokea somo kutoka Jukwaa la leo lililofanyika kwenye Hoteli ya Gold Crest mkoani Mwanza.

Burudani nayo haikukosa nafasi kwani vijana wa Rock city Band walimwaga raha....

Mc wa Jukwaa hilo Costantine Magavila akisalimiana na wadau walioalikwa kupokea somo.

Changamsha changamsha ya ChiaZZz kwa wadau wa jukwaa la leo lililofanyika kwenye Hoteli ya Gold Crest mkoani Mwanza.

ChiaZZz ya Leanne Martin-Pollock ambaye ni PR wa Trinity Promotion Ltd na wana habari Mwanza.

Huduma ziliboreshwa toka mlangoni.

Menyu ya mtikisiko dizaini ....

Baada ya jukwaa kumalizika Rock city Band walisababisha...

Tigo huduma.
Tigo ilianza biashara 1994 kama mtandao wa kwanza wa simu za mkononi Tanzania. Sasa inapatikana katika mikoa yote 26 Tanzania bara na Zanzibar. Tigo imejitahidi kuwa na ubunifu katika uendeshaji wa huduma zake za simu nchini Tanzania kwa kutoa huduma zenye gharama nafuu katika mawasiliano mpaka katika kutoa huduma za internet zenye kasi na huduma za fedha kwa njia ya simu kupitia Tigo Pesa.
Wadau wakijisevia.
Tigo ni sehemu ya Millicom International cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mikononi kwa gaharama nafuu na inapatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanayoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.