* Nyota wa Airtel Trace Music Stars apatikana Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imemtangaza rasmi mshindi wa shindano la Airtel Trace Music star, shindano lilidumu kwa muda wa miezi mitatu maalum kwa wasanii chipukizi kuweza kuimba na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi kama studio kwa lengo la kusaka na kuibua vipaji kwa wanamuziki chipukizi nchini.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga alisema"Leo tunayofuraha kubwa kumtangaza mshindi wetu wa shindano la Airtel Trace Music Stars mara baada ya kuchaguliwa na majaji na kupigiwa kura na watanzania "Washiriki watano ni kati ya wengi waliothubutu kuonyesha uwezo wao wa kushiriki kwa kupiga simu, kuimba na kutuma nyimbo zao na hatimae majaji wamesikiliza vipaji vyao kama walivyoimba na kuwachagua kuingia tano bora (top 5)" alifafanua Muga.
Washiriki waliokuwa wamebahatika kuingia tano bora ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182), Christopher Kihwele (5510050), Tracy Eminence (55100420), Beautus Henry (55100106) na Rose Mbuya (55100366) Mshindi wetu ni Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki (55100182) ambae amechaguliwa na majaji wetu pamoja na kupigiwa kura nyingi na wananchi Zawadi yake ni milioni Tshs 50mil, na pia atapata fursa ya kwenda kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Stars ya Afrika Nairobi Kenya yanayoshirikisha nchi 13 barani Afrika ambapo pia mshindi atakaepatikana atarekodiwa nyimbo zake katika studio za kimataifa nchini uingereza, na kupewa mafunzo toka kwa msanii nguli wa Afrika Akon.
Nchi nyingine zinazoshiriki mashindano haya na zitakazotoa jumla ya vijana 13 barani Afrika ni pamoja na Kenya, Uganda Zambia, Madagascar, Malawi, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, The Democratic Republic of Congo (DRC), na Gabon
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.