BAADHI
ya Waandishi wa Habari na Watoa huduma mkoani Mwanza wamekutanishwa katika
Mafunzo ya kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia yanayotolewa na Shirika
lisilo la kiserikali la kutetea haki za Wanawake na Watoto la KIVULINI.
Mafunzo
hayo yanatolewa kipindi hiki ambapo Mikoa ya kanda ya Ziwa inatajwa kuongoza
nchini kwa vitendo vya Ukatili hususani wa kijinsia. (BOFYA PLAY KUMSIKILIZA)
Meneja wa mradi wa SASA wilayani Misungwi Bi.Juliana Myeya akiwasilisha maelezo kuhusu mradi, malengo, utafuti, changamoto na jinsi utakavyofanya kazi katika awamu ya pili na ya tatu. |
Maimuna
Kanyamala ni Muasisi wa Shirika la KIVULINI anabainisha hali ya kijinsia ilivyo
katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. (BOFYA PLAY KUSIKILIZA)
Sehemu ya wadau na wawakilishi wa mashirika mbalimbali katika mafunzo. |
Kwa
upande wake mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza, Mrakibu
Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Jonathan Shana ametumia ufunguzi wa mafunzo hayo
kutoa salamu kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya Ukatili. (BOFYA PLAY MSIKILIZE)
Sehemu ya wadau na wawakilishi wa mashirika mbalimbali katika mafunzo. |
Suala
la katiba iliyopendekezwa ikisubiri kupigiwa kura nalo halikusahaulika
ambapo Serikali imeombwa kuharakisha zoezi la kuchapisha katiba
iliyopendekezwa na kuisambaza mapema ili wananchi wapate muda wa kutosha
kuipitia kabla ya kuipigia kura ili kubaini kama
kuna mapungufu hususani vipengele vilivoongezwa kumpa nafasi zaidi
mwanamke. (BOFYA PLAY SIKILIZA)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.