ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 18, 2018

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA 5 AJINYONGA SENGEREMA.


Mwanafunzi wa Kidato cha Tano, Shule ya Sekondari ya Sengerema aitwaye Ayoub Yahya Petro (19), mwenyeji wa Kyerwa mkoani Kagera, amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya chandarua aliokua ameifunga kwenye mti uliopo pembeni ya uwanja wa mpira wa shule hiyo, iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.

Tukio hilo limetokea leo Oktoba 18, 2018 majira ya saa 12: 00 asubuhi, hii ni baada ya wanafunzi wenzake kupita eneo la uwanja wa shule kisha kuona mwili wa marehemu Ayoub aliyekuwa akisoma mchepuo wa PCB, ukiwa unaning’inia juu ya mti na kutoa taarifa kwenye uongozi wa shule ambao ulifikisha taarifa hizo kituo cha polisi.

Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya DDH Sengerema kwa ajili ya uchunguzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya mazishi.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesema bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na kwamba linatoa wito kwa wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.