ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 18, 2018

"LAITI KAMA NINGEMSIKILIZA MWANANGU YASINGENIKUTA HAYA" ASEMA BABA WA MMOJA WA WATOTO 6 WALIOFARIKI KWA RADI GEITA



GSENGOtV

Baba wa marehemu Yusra Ayuni aitwaye Auni Idrisa Ramadhani anasema tukio la kifo cha mwanaye mara ya kwanza wakati akipata taarifa alilipokea kwa mshtuko mno.

"Ingawa kifo si jambo geni lakini mazingira yake wakati mwingine yanaweza kukufanya ukajiuliza maswali mengi na kuishia kujilaumu" Anasema Auni
Marehemu Yusra Ayuni mwanafunzi wa darasa la pili aliyefariki kwenye ajali ya radi shule ya msingi Emaco iliyopo mkoani Geita..

Na kisha kuongeza "Siku ya tukio Yusra alikuwa akijibizana na mama yake, kwamba yeye hataki kwenda shule......lakini mwishoweikabidi aende.........Labda asingeenda asingefariki......"


Wengi wamejitokeza nyumbani kwa wazazi wa Marehemu Yusra Ayuni mwanafunzi wa darasa la pili aliyefariki kwenye ajali ya radi shule ya msingi Emaco iliyopo mkoani Geita kwaajili ya shughuli za mazishi..
Taratibu zinaendelea nyumbani hapa.
Akinamama wakiwa kwenye majonzi kwenye ibada ya marehemu Yusra Ayuni..
Mazishi yamefanyika leo kwenye makaburi ya waislamu Mkoani Geita. 
Sehemu ya wahudhuriaji katika mazishi ya Marehemu Yusra.
Hatua ya mazishi ikiendelea kumzika marehemu Yusra Ayuni mwanafunzi wa darasa la pili aliyefariki kwenye ajali ya radi shule ya msingi Emaco iliyopo mkoani Geita..
Safiri salama.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.