ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 18, 2018

MKUU WA SHULE WALIOFARIKI WANAFUNZI 6 KWA RADI ANASEMA ALIGUNDUA TUKIO HILO MARA BAADA YA KUHISI HARUFU ILIYOMTATIZA.



GSENGOtV

Taarifa ya vifo vya wanafunzi 6 wa shule ya msingi Emaco mjini Geita na wengine 25 kujeruhiwa, baada ya kupigwa na radi wakiwa darasani imestua wengi.

Jembe fm kupitia kipindi chake cha #KAZINANGOMA mapema kabisa leo imekuwa mjini Geita na kupeperusha matangazo LIVE kutoka eneo la tukio.

Sanjari na kutoa pole, kungumza na Uongozi wa Shule, Waathirika na familia zilizopoteza watoto pamoja pia tumefanya juhudi kujaribu kuona nini kifanyike kwa majanga haya yasije jirudia.

Kuhusu tukio:- Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Octavian Lawrian anasema wakati akikagua mazingira ya shule kuhakikisha kwamba wanafunzi hawachezi kwenye mvua aligundua tukio hilo mara baada ya kuhisi harufu iliyomtatiza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.