ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 17, 2018

HIVI NDIVYO MILA NA DESTURI ZINAVYOCHANGIA ONGEZEKO LA MIMBA ZA UTOTONI NA KUSHUKA KIWANGO CHA ELIMU WILAYANI TARIME



GSENGOtV

Mila na Desturi zinatajwa kuchachangia kwa kiwango kikubwa mimba za utotoni na kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani Tarime nini sababu, wapi tunakosea kama jamii?

Wakizungumza wakati wa mkutano baina yao na Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana la KIVULINI, wazee hao wameahidi kumfichua yeyote atakayebainika kumkeketa mtoto wa kike ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Wazee wanaosimamia mila na desturi kutoka koo 12 za Kabila la WAKURYA Wilayani TARIME Mkoani MARA pamoja na Mangariba kutoka koo hizo wametangaza kuachana na ukeketaji wa watoto wa kike baada ya kutambua kuwa vitendo hivyo vinamuondolea haki utu na heshima mtoto wa kike.


Madiwani,Viongozi wa Dini, Wanaharakati, Wazee wa Mila, Mangariba, Viongozi wa kata pamoja na Maafisa elimu wilayani Tarime wacha wenyewe wafunguke. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.