Kwa mujibu wavyombo vya habari vya ndani zaidi ya watu 6 wahofiwa kufariki na wengine zaidi ya 86 kujeruhiwa baada ya treni kuacha njia karibu na mji mkuu wa Morocco, Rabat, siku ya jumanne.
Ajali ilitokea katika mji wa Sidi Bouknadel uliopo katikati ya Rabat na mji wa kaskazin magharibi wa Kenitra.
Picha zilizosambazwa kwenye kurasa za kijamii zinaonyesha mabehewa yakiwa yamepinduka, pia baadhi ya video zinaonyesha raia wema wakijaribu kutoa msaada.
"Uchunguzi umeanza kufanyika kubaini chanzo cha ajali hiyo" ilisema taarifa iliyotolewa na mahakama kuu ya Morocco.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.