ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 17, 2018

MHE.PROF. IBRAHIM HAMIS JUMA, JAJI MKUU WA TANZANIA ATEMBELEA MAHAKAMA YA WILAYA YA KWIMBA..


 NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. IBRAHIM HAMIS JUMA leo ametembelea mahakama ya wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza, kujionea mazingira na changamoto zilizopo ainazokwamisha utendaji katika maeneo mbalimbali  ya mahakama ya mwanzo wilayani humo.

Akiwa katika ziara yake ya siku 4 ya kikazi mkoani hapa, Prof. IBRAHIM, amekutana na watumishi wa mahakama hizo ili kupokea mawazo na na kuona jinsi gani Serikali inaweza kutatuwa changamoto zinazowakabili.

Kwenye ziara yake hiyo Prof. IBRAHIM HAMIS JUMA, amepokelewa na mwenyeji wake Mhe. Shanif Mansoor, Mbunge wa Jimbo la Kwimba na Mwenyekiti wa ulinzi na usalama ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo Senyi Ngaga.

 Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akiteta jambo na  mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe.SHANIF MANSOOR,

Mmoja kati ya watendaji wa mahakama wilayani Kwimba akitoa maelekezo.
 Moja kati ya changamoto alizozibaini kwenye ziara hiyo ni pamoja na upungufu wa watumishi, uchakavu wa miundombinu, uhaba wa majengo ya mahakama na ofisi za watendaji wake pamoja na vitendea kazi kulingana na kasi ya maendeleo ya teknolojia. 

, Mhe. Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Hamis Juma akipata picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.