ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 17, 2018

MUUNGANO WA MACHINGA MKOA WA MWANZA WAMTEMA KATIBU MWENEZI WAKE.



GSENGOtV

UONGOZI wa Machinga mkoa wa Mwanza kupitia Kamati Tendaji umeamua kuwafukuza moja kwa moja kwenye taasisi ya Muungano wa Machinga, Athuman Ujiji ambaye alichaguliwa kama Katibu Mwenezi katika Muungano wa Machinga.

Hatua hiyo inakuja baada ya Ujiji kunukuliwa akitoa shutuma waziwazi mbele ya vyombo vya habari akisema kuwa Viongozi hao walipokea Mlungula wa Milioni 12 toka kwa familia ya Mathias Charles Ndetto ili kuhalalisha hatua za kuwaondoa wamachinga kwenye eneo la Sahara.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kushuhudia tukio la Muungano wa Wamachinga kukabidhi rasmi eneo la kiwanja 195 A BLOC U  Rwagasore amesema tayari wamempiga barua Mwenezi huyo.

Viongozi wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza pamoja na Afisa Mtendaji wa Kata ya Pamba Jonas Mgisha (wa pili waliosimama mbele) wakipeana mkono na Mmiliki wa Eneo hilo Charles Ndetto mara baada ya Machinga kuondoka rasmi.

AUDIO HAYA HAPA MAJIBU YA ATHUMAN UJIJI 


 

Picha ya pamoja Viongozi wa Muungano wa Machinga Mkoa wa Mwanza pamoja na Afisa Mtendaji wa Kata ya Pamba Jonas, Mmiliki wa Eneo hilo Charles Ndetto na baadhi ya wanachama wamachinga..

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.