Mkuu wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Senyi Ngaga, ameambana na mbunge wa jimbo la kwimba Mhe.SHANIF MANSOOR, kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Mwamashimba kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa na Serikali kwa kiasi ya shilingi milioni 400.
Licha ya kujitolea nguvu kazi ili kukamilisha mradi huo kwa wakati Mhe. NGAGA amewataka wananchi wa Mwamashimba kusimamia kimilifu mradi huo, katika kuulinda kuondokana na uharibifu wa wachache wenye nia ovu.
NGAGA, amepongeza Mhe.SHANIF MANSOOR, kwa jitihada zake binafsi za kuisaidia Serikali kuchochea maendeleo ya Jimbo lake akisema kuwa hakika huo ndiyo uzalendo ambao iwapo ungeigwa na watanzania wengi taifa hili lingekuwa kama peponi.
Sanjari na kuahidi kusimamia vyema miradi ya maendeleo, wananchi wa Mwamashimba wamepongeza juhudi za Mhe. SHANIF, kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ikiwa ni pamoja na kufungua barabara za ndani na zinazoingia katika tarafa ya Mwamashimba, hali ambayo wameitaja kuwa itachochea kasi ya maendeleo katika jimbo lao.
Uongozi ni mfano safu ya viongozi walioambatana kwenye ukaguzi ilifanya usaidizi kupanga matofali ya ujenzi wa kituo cha afya Mwamashimba, huku akishuhudiwa na Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe.SHANIF MANSOOR na wadau wengine.
Hatua za ukaguzi zikiendelea.
Wananchi wa kata ya Mwamashimba wakiwa kwenye kusanyiko la kujadili shughuli za maendeleo yao.
Mbunge wa Kwimba Mhe.SHANIF MANSOOR akizungumza na wananchi kata ya Mwamashimba mara baada ya kutembelea kituo cha Afya Mwamashimba kujionea maendeleo ya ujenzi.
Mkuu wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Senyi Ngaga, akizungumza na wananchi kata ya Mwamashimba.
Safu ya mbele ni akinamama na nyuma akinababa kwa umakini ndani ya kusanyiko wakifuatilia kinachoendelea.
Mkuu wa wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Senyi Ngaga, akizungumza na wananchi kata ya Mwamashimba.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.