Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mtambo wa kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018. Mwingine Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh Pandit. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakifatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), alipotembelea na kukagua kiwanda cha Darsh jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
Na Mathias Canal-WK, Mseke-Iringa
Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt
Charles Tizeba (Mb), amewataka wakulima wa nyanya Mkoani Iringa kuchangamkia
fursa ya kuongeza uzalishaji wa nyanya ili kuakisi uhitaji wa viwanda vya
nyanya ikiwa ni pamoja na kiwanda cha Darsh chenye uwezo wa kusindika Tani 250
za nyanya kwa siku.
Waziri Tizeba ametoa mwito huo
jana Octoba 18, 2018 wakati akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha
Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya
ya Iringa.
Kiwanda hicho kinafanya shughuli
za ukusanyaji wa nyanya kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa na mikoa ya
jirani na kufanya usindikaji wa nyanya ambapo hupeleka kiwanda cha Arusha kwa
ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na nyanya ambazo huuzwa ndani na nje
ya nchi.
Waziri Tizeba, aliwataka
wakulima hao kujiunga kuanzisha kikundi cha ushirika ili kuwa na urahisi wa
mikopo ili kuwezesha uwezo wa uwekezaji kupitia kilimo cha umwagiliaji
kitakachoongeza tija katika kipato chao na jamii kwa ujumla.
“Wakulima wa nyanya hapa
Igwachanya na hata katika maeneo mengi nchini wanalima kwa kutegemea mvua na
uzalishaji huwa mdogo na usiokidhi mahitaji ya soko hivyo nawasihi kuongeza
uzalishaji wa nyanya kwani soko la uhakika lipo” Alikaririwa Dkt Tizeba
Kadhalika, Waziri wa kilimo aliutaka
uongozi wa kiwanda hicho kuongeza wigo wa ununuzi wa nyanya katika mikoa
mingine ya uzalishaji ikiwemo mkoa wa Dodoama na Singida.
Awali akisoma taarifa ya kiwanda
hicho mbele ya mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh
Pandit ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. John
Pombe Magufuli kwa kuhimiza sera ya uchumi wa viwanda kwa kuendelea kuboresha
mazingira ya uwekezaji na kuendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto chache
zinazojitokeza hivyo kuendelea kulinda maslahi mapana ya Taifa.
Alisema uanzishwaji wa kiwanda
hicho ulitokana na ushawishi uliopatikana kutoka kwenye muunganiko wa
wajasiliamali vijijini (MUVI) na Techno Serve walipotembelea kiwanda cha Darsh
Mkoani Arusha.
Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa
Mhe Richard Kasesela alimpongeza waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba
kwa kutenga muda wake na kukubali kufanya ziara Wilayani Iringa ili kubaini
changamoto zinazowakabili wakulima wa nyanya nchini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.