Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti waBaraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati ya Uzinduzi wa Kampeni Maalumu ya Usalama Barabarani na Udhibiti wa Ajali katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo VisiwaniZanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Jang’ombe, Aisha Abdallah Haji, akiulizaswali linalohusiana na uvukaji wa barabara kwa watu wenye ulemavu wakatiwa Uzinduzi wa Kampeni Maalumu ya Usalama Barabarani na Udhibiti waAjali katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, iliyozinduliwa leo Naibu Waziriwa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa laUsalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), VisiwaniZanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Wanafunzi wakifurahia jambo wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndaniya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza baada ya kuzinduaKampeni Maalumu ya Usalama Barabarani na Udhibiti wa Ajali katikaUwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo Visiwani Zanzibar. Picha na Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti waBaraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni,akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jang’ombe, Tiffy Mustafa(kushoto), moja ya kikoti maalumu watakachokua wanavaa wanafunzi watakaoteuliwa kuwasaidia wenzao kuvuka barabara baada ya kuzinduaKampeni Maalumu ya Usalama Barabarani na Udhibiti wa Ajali katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo Visiwani Zanzibar. Picha na Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi
Mkurugenzi wa Taasisi inayojishughulisha na masuala ya usalama barabarani, Pily Hamisi Layda (kushoto) akimkabidhi Naibu Waziri waMambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa laUsalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, mpango kazi wa KampeniMaalumu ya Usalama Barabarani na Udhibiti wa Ajali iliyozinduliwa katikaUwanja wa Skuli ya Jang’ombe, leo Visiwani Zanzibar. Picha na Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, amewatadharisha wamiliki wa shule zinazotumia magari mabovu kubebea wanafunzi ikiwa ni kinyume na sheria za usalama barabarani hali ambayo inaweza kupelekea ajali.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampeni Maalumu ya Usalama Barabarani na Udhibiti wa Ajali katika Uwanja wa Skuli ya Jang’ombe, Naibu Waziri Masauni aliwataka wamiliki wa shule kuhakikisha wanatumia mabasi imara ili kuepusha ajali na kuwaasa madereva wa magari hayo kufuata sheria za barabarani “Wamiliki wa shule wanatakiwa wafuate sheria kwa kuacha kutumia mabasi mabovu na kujaza wanafunzi kupita kiasi na tutatumia kikosi cha usalama barabarani kuhakikisha wanafunzi wanakua salama muda wote wakiwa wanaenda shule na kurudi nyumbani.
“Nawaagiza askari wa usalama barabarani kusimamia sheria ili wamiliki watakao kiuka sharia hizo waweze kuchukuliwa hatua pamoja na madereva watakaobainika kuendesha magari mabovu ambayo ni hatarishi kwa wanafunzi,” alisema Masauni
Akitoa ripoti ya matukio ya ajali za barabarani Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Shukuru Amir Ally alisema jumla ya ajali 229 zimeripotiwa ndani ya mwaka huu tofauti na mwaka 2017 ambapo jumla ya ajali 391 zikiripotiwa huku akitoa siri ya kupungua kwa ajali hizo ni ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wadau wa usalama barabarani.
Akisoma risala ya uzinduzi huo Mkurugenzi wa Taasisi inayojishughulisha na masuala ya usalama barabarani ya New Vision, Pily Hamis Ladya alisema wamedhamiria kufikia mikoa yote ya Zanzibar na katika awamu hii ya kwanza wanaanza na shule kumi huku akiahidi kuzifikia shule zote katika kutoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi.
“Tunategemea kutoa elimu hii ya usalama barabarani ili kuweza kuwaepusha na kuwalinda wanafunzi wetu na majanga ya barabarani ili waweze kwenda shule na kurudi nyumbani salama,” alisema
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.