ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 15, 2011

YEHOVA YU HAI LIVE TOUR ILIVYOFANA MWANZA

Mwimbaji mahiri wa kimataifa wa muziki wa injili John Lisu akimtambulisha Mke wake Nelly Lisu katika Tamasha lililopewa jina la JEHOVA Yu Hai Tour lililofanyika tarehe 6 November 2011, ambapo Lisu aliongozana na Timu ya Wapiga Vyombo na waimbaji kutoka jijini Dar.

Mimi hupenda kumwita Dogo lakini ni mmoja wa waimbaji anayekuja kwa kasi katika Tasnia ya muziki wa injili na pia mtangazaji wa Radio ya kikristo ya 91.9 ALIVE FM ya Jijini mwanza Adolph Robert Nzwalla akihusika kikamilifu kuhakikisha jina la Yesu linainuliwa.

Wakati wa kuliombea taifa la Tanzania ilikuwa ni tofauti na tulivyozoea kwani watu waliimba wimbo huu kwa njia ya kuabudu na watu walibubujikwa hisia.

Mrs Matata na mwanae Kivila Matata nao waliguswa na roho kuhudhuria tamasha hili la aina yake lililofanyika kwa mara ya kwanza jijini hapa.

Bishop Murisa Akifanya maombezi.

Full upako

Watu wakimwadhimisha Mungu.
CHANZO: http://www.vipajihalisi.blogspot.com/

MAPIGANO YA KIKABILA NCHINI LIBYA

Kumekuwepo na mapambano ya siku kadhaa kati ya makundi yanayokinzana katika mji wa mwambao wa Zawiya nchini Libya ambapo takriban watu 7 waliuawa.
Mwandishi wa BBC Karen Allen akiwa Libya anasema jamii zinazopingana zimekua zikipigania eneo ambalo zamani lilidhibitiwa na wafuasi wa kanali Gaddafi.

Hata hivyo serikali ya mpito imesema kwamba mapigano hayo yalisuluhishwa.

Wachambuzi wanasema mapigano hayo yanazusha masuala kadhaa kuhusu hali ya utulivu baada ya kuondoka kwa Gaddaffi nchini Libya.

Libya bado inakabiliwa na changamoto za kuenea silaha na vikundi vya watu wenye silaha baada ya uasi uliosababisha kuporomoka kwa utawala wa Kanali l Muammar Gaddafi.

Kiongozi wa utawala wa mpito Mustafa Abdul-Jalil alisema baraza la taifa la mpito limewakutanisha wazee kutoka maeneo yanayogombaniwa ya Zawiya na maeneo ya karibu ya makabila ya Warshefana - na kwamba mzozo huo umesuluhishwa mwishoni mwa wiki..

Wapiganaji toka Zawia wakifurumisha roketi kuelekea eneo la makazi ya watu wa kabila la Warcafana umbali wa maili 25 toka mji wa Tripoli.
Hata hivyo baadhi ya watu wamearifu kuwa mapigano bado yalikuwa yanaendelea wakati akiongea.

Taarifa zaeleza kuwa mapigano yalianza pale wapiganaji kutoka Warshefana walipoweka kizuizi cha barabarani katika njia panda karibu na Zawiya, na kuwatambia wapiganaji kutoka mjini humo.

Wapiganaji kutoka Zawiya waliwashutumu wale kutoka Warshefana kuwa na ufungamano na utawala wa zamani

CHANZO bbc Swahili.

Monday, November 14, 2011

JAPO KIDEO: MAFURIKO MWANZA AIRPORT.

Mvua kubwa iliyonyesha leo asubuhi jijini Mwanza japo mwisho mwisho wakati hali ilipotulia.

HALI YA SASA 19:30
Hali ya sasa ni shwari mara baada ya mafuriko makubwa yaliyotokea na kusababisha kusitishwa kwa safari zote za anga.

Safari za ndege zimerejea kama kawaida baada ya safisha safisha ya njia za ndege kufanyika. Precission Air ile boing imefika na kuondoka, Precission ATR 42 nayo imeland na kuondoka na abiria salama salmini.

Nayo ndege ya Kahama Mining iliyokwama kutua wakati wa gharika na kuamua kurejea kahama imetua muda mrefu uliopita na kusepa... ndege inayosubiriwa kwa sasa ni 540..
"Siyo shambani bali naelekea uwanja wa ndege"- Wazee wa safisha safisha.

MAFURIKO UWANJA WA NDEGE MWANZA YASABABISHA UWANJA KUFUNGWA KWA MUDA, ABIRIA WASHINDWA KUSAFIRI

Mvua kubwa iliyonyesha leo jijini Mwanza kwa takribani masaa manne imeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za usafiri na usafirishaji kwa njia ya anga.

Hali halisi....hatoki mtu...!!

kwasababu za kiusalama hakuna ndege iliyoruhusiwa kutoka au kuingia Air port Mwanza.

Hali ilikuwa mbaya zaidi majira ya saa mbili asubuhi ambapo maji mengi yaliyokuwa yakitiririka kutoka eneo la mwinuko kaskazini mwa kiwanja cha ndege Mwanza, yalisababisha taswira ya uwanja kubadilika na kuwa kama sehemu ya mto mkubwa unaotiririsha maji kuelekea ziwa victoria.

Pichani ni kama ndege iliyogota katikati ya shamba la mpunga kumbe laaa!! ni ndege iliyo katika eneo stahiki la maegesho ya ndege.

Wafanyakazi mbalimbali kiwanjani hapo wakishughulika kusafisha njia za ndege mara baada ya magugu na tope jingi kutanda eneo hilo.

Kikazi zaidi...kama shambani vile.

Hawa ndege sijui walitoka wapi!!! Naskia ni hatari sana kwa ndege ndogo za abiria.

Chekshia ngazi za ndege....

Wafanyakazi wa idara tofauti kiwanjani hapo wakihaha kuzima swichi za umeme kiwanjani hapo mara baada ya kina cha maji kuanza kupanda taratibu kikitishia usalama.

Wafanyakazi sekta ya mizigo walifanya kazi ya ziada kunusuru mizigo ilokuwa tayari imepakiwa kitengo cha mizigo isilowe.

Mara baada ya maji kupungua unaweza kuona jinsi miundo mbinu hasa njia za ndege ilivyoathirika.

Pata picha kama ndege zingeruhusiwa kuondoka au kutua wakati wa mafuriko ile hali tayari njia zandege zishaharibika......!!!!!???!!.

Hapa unaambiwa ni hali imetulia kwa Ofisi zetu kiwanjani.

LOWASA: TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA WA TANZANIA NI BOMU LINALOSUBIRI KULIPUKA.

Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyayi Lowasa amesema kuwa pengo kubwa la vijana ambao hawana ajira ni bomu kubwa na zigo jingine kwa Serikali ya awamu ya nne endapo halitadhibitiwa mapema kwa kupatiwa ajira stahiki. Mbunge wa Monduli Edward Lowasa akipeana mkono na baadhi ya wanafunzi wa shule ya wasichana Loreto mara baada ya kupokea mchango wa shule hiyo kwa ujenzi wa wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato jijini Mwanza.

Lowasa ameyasema hayo jana jijini Mwanza wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato kabla ya kuanzisha harambee maalum ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.

Amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2006 unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 12 ya vijana hawana ajira na wengi wa vijana hao wako mijini, asilimia 15 ya vijana nchini kati ya milioni 25 za vijana ndio wenye ajira, ilihali asilimia 70 ya vijana wenye umri kati ya miaka 13 -34 ni kundi kubwa ambalo ni tegemezi na halina ajira na hii ni kati ya nguvu kazi ya vijana milioni mbili na nusu ambao wako mijini na hawana ajira.

Amefafanua kuwa wakati hali hiyo ikitokea vijana 850,000 ambao wamekuwa wakihitimu elimu ya msingi, sekondari na vyuo wakiwa tayari kuingia kwenye soko la ajira lakini inasikitisha kati ya hao, ni asilimi 5 tu ndio wanaopata ajira ya kudumu, huku asilimia 35 ikijikita katika kilimo ambacho bado kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo zile za uhaba wa pembejeo.

Amewataka watanzania wote kushirikiana na serikali kuhakikisha kuwa inawekwa mipango madhubuti kulinusuru kundi hilo kubwa la vijana wenye utayari wa kuingia kwenye ajira.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria harambee hiyo ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa zamani Nyamagana Lawrence Masha, Mbunge wa Rolya Lameck Airo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Christopher Mwita Gachuma, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega(CCM) Dk. Raphael Chegeni na Mbunge wa sasa wa Nyamagana(Chadema) Ezekiah Dibogo Wenje.

Kwa upande wa uwakilishi wa Serikali uliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Said Amanzi na baadhi ya wafanyabiashara maarufu wa mikoa ya kanda ya ziwa na baadhi wazee maarufu.

Katika harambee hiyo ya kusisimua iliyoongozwa na Mbunge wa Monduli Mh.Edward Lowasa aliyetoa shilingi milioni 10 kama mchango wake, jumla ya shilingi milioni 200 zimepatikana hivyo kuvuka lengo la shilingi milioni 150, kumalizia Ujenzi wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato Mwanza.
Mazingira ya kanisa la nyakato.

Sunday, November 13, 2011

LOWASA AFANIKISHA KUVUKA LENGO UJENZI KANISA LA ROMAN CATHOLIC PAROKIA YA NYAKATO MWANZA, AHAMASISHA WAUMINI NA MARAFIKI ZAKE WACHANGA MILIONI 200

Jumla ya shilingi milioni 200 zimepatikana leo na kuvuka lengo la shilingi milioni 150, katika harambee ya kusisimua ya Kumalizia Ujenzi wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato jijini Mwanza harambee iliyoongozwa na Mbunge wa Monduli Mh.Edward lowasa.

Waziri mstaafu ambaye ni mbunge wa Monduli Edward Lowasa akipokea Cheti cha kutambua mchango wake kusimamia vyema harambee za jamii na zawadi ya mbuzi toka kwa kamati ya ujenzi kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato Mwanza, mbuzi alinadiwa na kununuliwa na Papaa King kwa dola 100.

ONE LOVE Wenje $ Masha.
Miongoni mwa viongozi walioitikia harambee hiyo ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Nyamagana Lawrence Masha (kulia) aliyechanga shilingi milioni 3.5, kisha milioni 1.5 toka kwa marafiki zake na laki moja aliyomwongezea mbunge Mama Hewa, ile hali Mbunge wa sasa Ezekiel Wenje (kushoto) kwa upande wake alichanga shilingi milioni 1.5.


Akinamama walisimama kidete kuhakikisha lengo linafikiwa hapa Mama Kemilembe akiwasilisha mchango wake kwa mgeni rasmi.

"Kaka zimetimiaa" ni Mbunge wa Rolya Lameck Airo (shoto) na mfanyabiasha maarufu jijini Mwanza 'Six'.

Sehemu ya waumini waliofurika kwa wingi kufanikisha harambee hiyo.

Ni kanisa kubwa lililowekewa lengo na waumini wake kukamilika ujenzi na watu kusali ndani mwake katika ibada ya sikukuu ya Krismas ya mwaka huu 2011.

Marafiki wa mh. lowasa, Mkurugenzi wa Gold Crest Mr. Manga, Papaa King na Naftari Njoroge walijitutumua kweli kwenye harambee hiyo.

Mkazi wa jiji Mzee Ramadhani naye alialikwa kwenye harambee hiyo, hapa akimkabidhi Cash' shilingi laki 5 mchangishaji namba mbili mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Christopher Mwita Gachuma ambaye ni miongoni mwa waliojitokeza kwa dhati kufanikisha.

Lowasa alitumia ufundi mkubwa kuendesha harambee hiyo, pichani Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje akiwa kikaangoni na hatimaye aliwasilisha fungu lake na ahadi za marafiki zake walio mbali.

Wakurungenzi wa EF DOOR nao hawakuiangusha safu, walishiriki kikamilifu.

Mbunge wa Rolya, bw. Lameck Airo upande wake alichangia kiasi cha shilingi milioni 5.

Picha ya pamoja mgeni rasmi na Kwaya kuu ya kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato Mwanza.

Saturday, November 12, 2011

AMANI NA UTULIVU WAREJEA GHAFLA MKOANI MBEYA NA SHUGHULI KUENDELEA KAMA KAWAIDA KUANZIA LEO, MMTU MMOJA AFARIKI KATIKA VURUGU ZA SIKU 2.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama katika jengo la kitega uchumi la OTTU lililopo stendi ya magari madogo ya abiria(daladala), mara baada ya Mbunge Mbilinyi kuhutubia wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama mwenye shati la miraba ya samawati(Katikati) katika picha ya pamoja kabla ya Mheshimiwa Mbunge Joseph Mbilinyi Kuhutubia.

Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi akiwasihi wananchi kuwa watulivu na kwamba mgogoro umekwisha na utatuliwe kisayansi badala ya kisiasa na pia amewapongeza machinga kwa utulivu waliouonesha bila kupora bidhaa madukani.

Halaiki ya wananchi waliofika kuusikiliza mustakabali wa wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga kuendelea na biashara zao katika maeneo yao ya awali, wakati utaratibu wa maeneo ya kufanyia biashara ukiandaliwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.

Wananchi wakirudi makwao kwa furaha baada ya mgogoro uliodumu kwa siku mbili kumalizika, baada ya hotuba ya Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Bwana Joseph Mbilinyi.

Picha zote na:
http://www.mbeyayetublog.blogspot.com/

TABORA YAKUMBWA NA UHABA WA MAFUTA IKIWA LEO NI SIKU YA NNE TATIZO LAWA KUBWA

Uhaba wa mafuta katika mkoa wa Tabora na Hivi ndivyo hali ilivyo katika pita pita za Latest news Tz na kujionea mstari mrefu watu wakisubiri kupata huduma ya mafuta. Hali hii ilianza kama siku nne zilizopita na kila siku kituo kimoja kinatoa huduma hiyo.

Picha na :
www.latestnewstz.blogspot.com

Friday, November 11, 2011

VURUGU ZA LEO WAMACHINGA SOKO LA MWANJELWA

Watu Mbali Mbali wakiwa wanakimbia ili kujiokoa na Hatari katika eneo hilo.

Wamachinga wakiwa Tayali kwa ajili ya Kupambana na FFU wakati wa tukio hilo

Baadhi ya wananchi wakiwa wameokoka katika eneo hilo


Wamachinga Mbali mbali wakikimbia katika eneo la tukio wakati wa machafuko hayo yamepamba moto

Polisi wakijalibu Kuzuia Ghasia katika eneo hilo na kufukuza Wamachinga.
Picha zote na:
http://www.latestnewstz.blogspot.com/