Mwandishi wa BBC Karen Allen akiwa Libya anasema jamii zinazopingana zimekua zikipigania eneo ambalo zamani lilidhibitiwa na wafuasi wa kanali Gaddafi.
Hata hivyo serikali ya mpito imesema kwamba mapigano hayo yalisuluhishwa.
Wachambuzi wanasema mapigano hayo yanazusha masuala kadhaa kuhusu hali ya utulivu baada ya kuondoka kwa Gaddaffi nchini Libya.
Libya bado inakabiliwa na changamoto za kuenea silaha na vikundi vya watu wenye silaha baada ya uasi uliosababisha kuporomoka kwa utawala wa Kanali l Muammar Gaddafi.
Kiongozi wa utawala wa mpito Mustafa Abdul-Jalil alisema baraza la taifa la mpito limewakutanisha wazee kutoka maeneo yanayogombaniwa ya Zawiya na maeneo ya karibu ya makabila ya Warshefana - na kwamba mzozo huo umesuluhishwa mwishoni mwa wiki..
Wapiganaji toka Zawia wakifurumisha roketi kuelekea eneo la makazi ya watu wa kabila la Warcafana umbali wa maili 25 toka mji wa Tripoli.
Hata hivyo baadhi ya watu wamearifu kuwa mapigano bado yalikuwa yanaendelea wakati akiongea.
Taarifa zaeleza kuwa mapigano yalianza pale wapiganaji kutoka Warshefana walipoweka kizuizi cha barabarani katika njia panda karibu na Zawiya, na kuwatambia wapiganaji kutoka mjini humo.
Wapiganaji kutoka Zawiya waliwashutumu wale kutoka Warshefana kuwa na ufungamano na utawala wa zamani
CHANZO bbc Swahili.
Tupe maoni yako
Albert! Libya is bound to fight for a very long time! Kwa sasa itazidi Somalia pole pole process inaanza.
ReplyDelete