ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 14, 2011

MAFURIKO UWANJA WA NDEGE MWANZA YASABABISHA UWANJA KUFUNGWA KWA MUDA, ABIRIA WASHINDWA KUSAFIRI

Mvua kubwa iliyonyesha leo jijini Mwanza kwa takribani masaa manne imeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za usafiri na usafirishaji kwa njia ya anga.

Hali halisi....hatoki mtu...!!

kwasababu za kiusalama hakuna ndege iliyoruhusiwa kutoka au kuingia Air port Mwanza.

Hali ilikuwa mbaya zaidi majira ya saa mbili asubuhi ambapo maji mengi yaliyokuwa yakitiririka kutoka eneo la mwinuko kaskazini mwa kiwanja cha ndege Mwanza, yalisababisha taswira ya uwanja kubadilika na kuwa kama sehemu ya mto mkubwa unaotiririsha maji kuelekea ziwa victoria.

Pichani ni kama ndege iliyogota katikati ya shamba la mpunga kumbe laaa!! ni ndege iliyo katika eneo stahiki la maegesho ya ndege.

Wafanyakazi mbalimbali kiwanjani hapo wakishughulika kusafisha njia za ndege mara baada ya magugu na tope jingi kutanda eneo hilo.

Kikazi zaidi...kama shambani vile.

Hawa ndege sijui walitoka wapi!!! Naskia ni hatari sana kwa ndege ndogo za abiria.

Chekshia ngazi za ndege....

Wafanyakazi wa idara tofauti kiwanjani hapo wakihaha kuzima swichi za umeme kiwanjani hapo mara baada ya kina cha maji kuanza kupanda taratibu kikitishia usalama.

Wafanyakazi sekta ya mizigo walifanya kazi ya ziada kunusuru mizigo ilokuwa tayari imepakiwa kitengo cha mizigo isilowe.

Mara baada ya maji kupungua unaweza kuona jinsi miundo mbinu hasa njia za ndege ilivyoathirika.

Pata picha kama ndege zingeruhusiwa kuondoka au kutua wakati wa mafuriko ile hali tayari njia zandege zishaharibika......!!!!!???!!.

Hapa unaambiwa ni hali imetulia kwa Ofisi zetu kiwanjani.

Tupe maoni yako

4 comments:

  1. Nice work Albert! You do a wonderful job maintaing this blog and thanks.

    ReplyDelete
  2. ASante kwa taarifa kaka. kazi kwao waliokuja kutalii na watoto wa watu

    ReplyDelete
  3. Jamani viwanja vyetu vya ndege vinatia aibu sana, huo mlango wa V.I.P sasa mmmmh!!! poleni kwa mvua ya jana.

    Ahsante pia kaka G kwa taarifa.

    ReplyDelete
  4. kazi nzuri sana kaka ila si airport tu je huko mabatini hali ilikuwa mbaya sana.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.