ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 14, 2011

LOWASA: TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA WA TANZANIA NI BOMU LINALOSUBIRI KULIPUKA.

Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyayi Lowasa amesema kuwa pengo kubwa la vijana ambao hawana ajira ni bomu kubwa na zigo jingine kwa Serikali ya awamu ya nne endapo halitadhibitiwa mapema kwa kupatiwa ajira stahiki. Mbunge wa Monduli Edward Lowasa akipeana mkono na baadhi ya wanafunzi wa shule ya wasichana Loreto mara baada ya kupokea mchango wa shule hiyo kwa ujenzi wa wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato jijini Mwanza.

Lowasa ameyasema hayo jana jijini Mwanza wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato kabla ya kuanzisha harambee maalum ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.

Amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2006 unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 12 ya vijana hawana ajira na wengi wa vijana hao wako mijini, asilimia 15 ya vijana nchini kati ya milioni 25 za vijana ndio wenye ajira, ilihali asilimia 70 ya vijana wenye umri kati ya miaka 13 -34 ni kundi kubwa ambalo ni tegemezi na halina ajira na hii ni kati ya nguvu kazi ya vijana milioni mbili na nusu ambao wako mijini na hawana ajira.

Amefafanua kuwa wakati hali hiyo ikitokea vijana 850,000 ambao wamekuwa wakihitimu elimu ya msingi, sekondari na vyuo wakiwa tayari kuingia kwenye soko la ajira lakini inasikitisha kati ya hao, ni asilimi 5 tu ndio wanaopata ajira ya kudumu, huku asilimia 35 ikijikita katika kilimo ambacho bado kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo zile za uhaba wa pembejeo.

Amewataka watanzania wote kushirikiana na serikali kuhakikisha kuwa inawekwa mipango madhubuti kulinusuru kundi hilo kubwa la vijana wenye utayari wa kuingia kwenye ajira.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria harambee hiyo ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa zamani Nyamagana Lawrence Masha, Mbunge wa Rolya Lameck Airo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Christopher Mwita Gachuma, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega(CCM) Dk. Raphael Chegeni na Mbunge wa sasa wa Nyamagana(Chadema) Ezekiah Dibogo Wenje.

Kwa upande wa uwakilishi wa Serikali uliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Said Amanzi na baadhi ya wafanyabiashara maarufu wa mikoa ya kanda ya ziwa na baadhi wazee maarufu.

Katika harambee hiyo ya kusisimua iliyoongozwa na Mbunge wa Monduli Mh.Edward Lowasa aliyetoa shilingi milioni 10 kama mchango wake, jumla ya shilingi milioni 200 zimepatikana hivyo kuvuka lengo la shilingi milioni 150, kumalizia Ujenzi wa Kanisa la Roman Catholic Parokia ya Nyakato Mwanza.
Mazingira ya kanisa la nyakato.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.