ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, May 17, 2012

TOWN STARS MABINGWA WA ESTER BULAYA CUP

Michuano ya Mbunge wa Viti maalum kupitia Umoja wa vijana CCM mkoani mara ESTHER BULAYA CUP imemalizika juzi ambapo michuano hiyo ilidumu kwa wiki mbili katika wilaya Bunda mkoani Mara, Katika michuano hiyo Mshindi alikuwa ni Town Star baada ya kuifunga timu ya Amani FC mabao 4-2 kwa mikwaju ya Penalti huku mshindi wa tatu Ikiwa Timu ya Polisi Fc.
Mbunge wa viti maalum kupitia Umoja wa vijana CCM mkoani Mara Ester Bulaya akikagua timu mabingwa Town Star kabla ya mchezo.

Mbunge wa viti maalum kupitia Umoja wa vijana CCM mkoani Mara Ester Bulaya akikagua timu mshindi wa pili Amani FC kabla ya mchezo.

Mashabiki wakisutumuka...

Mashabiki wa timu mabingwa wakimbeba shujaa wao.

Huyu ndiye kipa aliyekuwa mwiba katika fainali.

Katika michuano hiyo Mchezaji bora alikuwa Ramadhani Kifundu kutoka Aman Fc aliyepata zawadi ya shilingi ya shilingi 50,000/=

Katika michuano hiyo mabingwa Town Stars walipata zawadi ya shilingi 500,000/= na kombe.

Aman Fc wakaondoka na kitita cha shilingi 250,000/= Polisi Fc 150,000/= Mfungaji bora kutoka timu ya Balili fc 50,000/= Timu yenye nidhamu Mwembeni FC 50,000/=

BREAKING NEWS:PATRICK MAFISANGO WA SIMBA SC AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

Marehemu Patrick Mafisango (kwenye kiduara) katika picha ya pamoja na kikosi cha Simba enzi za uhai wake.
Mchezaji wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda kiungo mkabaji Patrick Mafisango amefariki dunia kwa ajali ya gari leo alfajiri katika eneo la Tazara jijini Dar es salaam.
Hili ndilo Gari alilopatanalo ajali marehemu Patrick Mafisango maeneo ya TAZARA jijini Dar.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba bwana Aden Rage amesema kuwa taarifa za awali juu ya chanzo cha kifo cha mchezaji huyo zinasema kuwa mchezaji huyo amekutwa na mauti akiwa anaendesha gari na kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki.

Msiba huu unakuja wakati kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda Milutin Sredovic 'Micho' akiwa amemteuwa kepteni wa zamani wa timu hiyo Hamada Ndikumana a.k.a 'Katauti' na Patrick Mafisango kujiunga na timu ya taifa hilo (AMAVUBI) kwaajili ya maandalizi ya nchi zitakazofuzu kwenda Brazil kwenye michuano ya Kombe la dunia 2014.

Kabla ya  kuichezea Simba mchezaji huyo alitokea Azam Fc ya jijini Dar es salaam.
Patrick Mafisango is dead.
Mwenyezi Mungu ilaze mahali pema peponi roho ya marehemu Patrick Mafisango.

Wednesday, May 16, 2012

RC MWANZA AWATAKA MA DC KUPAMBANA NA UFISADI WA FEDHA ZA UMMA KWENYE HALMASHAURI ZAO

Mkuu mpya wa wilaya ya Magu Jaqueline Liana akila kiapo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo leo katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa wilaya wa Kwimba Selemani Mzee Selemani akila kiapo cha utumishi mbele ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza huku akishuhudiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza akila kiapo cha utumishi kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo huku akishuhudiwa na Katibu Tawala mkoa Doroth Mwanyika.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akila kiapo cha utumishi mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza katika hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wapya saba wa wilaya za mkoa wa Mwanza uliofanyika leo.

Mkuu wa wilaya ya Misungwi wa zamani Mariam Lugaila akila kiapo mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza baada ya kuteuliwa tena kuwa mkuu wa wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Mary Tesha akila kiapo mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo.

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Karen Yunus akila kiapo cha utumishi wa umma.

Wanahabari nao hawakuwa nyuma kuwajibika katika tukio zima la kuapishwa wakuu wapya wa wilaya saba za mkoa wa Mwanza walioteuliwa hivi karibuni ambapo leo wameapishwa rasmi.
Picha ya pamoja ya wakuu wa wapya wilaya walioapishwa na viongozi waalikwa.

MISS ILEMELA KUFANYIKA GOLD CREST HOTEL MWANZA TAREHE 25/05/212

Baadhi ya warembo watakao shiriki kinyang'anyiro cha miss Ilemela kinachotarajiwa kufanyika tarehe 26/05/2012 kwa mara ya kwanza katika ukumbi mkubwa wa GOLD CREST HOTEL jijini Mwanza.

Ni warembo wenye sifa zote stahiki.

Flash ya warembo Kinyang'anyiro cha Miss Ilemela 2012.
Mkao binafsi kwenye flash..

Pamoja na kuwa na kipaji cha shughuli za ulimbwende pia mrembo huyu yu mtangazaji wa kituo cha Tv Barmedas jijini Mwanza.

W0w...!

Kuna TATIZO...!!?

Nice & Cool..

Fresh...

Crazy..

Chain..
Hapa ndipo mahala mrembo wa Miss Ilemela atapatikana ... Some body ameuliza kuhusu burudani jibu ni kwamba Rais wa Masharobaro Bob Junior atakisanukisha usiku huo ile mmmmmwaaa!!!

Tuesday, May 15, 2012

MADIWANI CHADEMA MWANZA WAGOMEA BAJETI YAO

Leo katika halmashuri ya jiji la Mwanza madiwani wa Chadema ambao ndiyo wanaunda Halmashauri ya Jiji la Mwanza, wamegoma kupitisha bajeti yao na kuzua mvutano huku wakiandikisha kupiga kura ya kutokuwa na imani na Meya Josephati Manyerere.

Madiwani 17 kati ya 29 wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutoka vyama vya Chadema, CCM na CUF wamesaini pendekezo la kutaka kumng'oa Meya wa Jiji hilo, Josephat Manyerere (Chadema) kwa madai ya kushindwa kuongoza Halmashauri hiyo.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuvurugika kwa kikao cha kupitisha Mpango wa Bajeti wa Halmashauri ya Jiji kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji baada ya mvutano uliodumu takribani saa tatu.

Madiwani hao wakiongozwa na Diwani wa Igoma, Adamu Chagulani (Chadema) wamesema wameamua kupiga kura ya kutokuwa na imani na Meya huyo kutokana na sababu mbalimbali. Chagulani alisema kuwa Manyerere, ameshindwa kusimamia Halmashauri na vikao kutoitishwa kwa wakati kutokana na kutoa maelekezo kuwa hakuna kikao kufanyika bila yeye kuwapo pia ameshindwa kuunganisha madiwani, hali ambayo imesababisha kuzorota kwa uhusiano baina ya madiwani na watendaji..

Sababu nyingine ni pamoja na kusaini mikataba kabla ya kupitishwa na Baraza la Madiwani, kukataa kusaini mikataba halali ambayo imepitishwa na Halmashauri ya Jiji, kupendelea kata yake katika miradi na kutumia madaraka yake vibaya.

Diwani wa Mkolani, Stanslaus Mabula (CCM) amemtuhumu Meya huyo kwa kutoa makabrasha ya rasimu ya Bajeti ya Jiji kwa watu wasiohusika katika kikao kisicho rasmi hivi karibuni.

Kwa upande wake Meya Manyerere amesema yuko tayari kuondolewa ikithibitika amevunja sheria na kanuni za kudumu za Halmashauri. Kabla ya uamuzi wa kumwondoa Meya, madiwani hao walikuwa katika malumbano na Meya huyo bila kujali itikadi za vyama kutokana na walichodai amekuwa akiwaburuza kwa kuahirisha kinyemela kikao cha Baraza kwa hofu ya kupigiwa kura hiyo.

BONGE WA CLOUDS APANDA MIGOMBA BARABARA YA MWANANYAMALA BAADA YA BARABARA HIYO KUTELEKEZWA

Mfanyakazi wa Radio Clauds FM, Said Mohamed 'Said Bonge' akipanda migomba kwenye mashimo ya barabara ya Mwananyamala Hospitali Dar es Salaam leo huku gari likipiata kando yake. Bonge alisema amechukua uwamuzi huo baada ya wahusika kushindwa kuyafukia mashimo hayo ambayo yamekuwa yakileta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Said Bonge akiendelea na shughuli ya kupanda migomba katika barabara ya Mwananyamala ambayo imeharibika vibaya huku wahusika wakiifumbia macho bila kuchukua hatua zozote za kuikarabati.
PICHA/HABARI na full shangwe

ELIMU BONGO IMEJAA UONGO

Ni WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA SHULE YA MSINGI MAKUMBUSHO LEO HII.
Matatizo ya elimu siyo mepesi na huwezi mtu kuyatatua kwa kutoa majibu mepesi. Unahitajika utafiti ambao utayaanisha matatizo yenyewe kwa vipengele, chanzo chake na namna ya kuyatatua, ili hatimaye tuweze kutoa elimu inayoweza kuitwa elimu anafafanua Ni jambo zuri Serikali inapofanya juhudi kuhakikisha watoto wanaenda shuleni, lakini wanapofika huko wanakutana na changamoto zinazofanya wasiweze kupata elimu bora bali bora elimu.

Changamoto ziko nyingi mojawapo ni ukosefu wa vifaa vya kufundishia, kujifunzia, mazingira duni na ukosefu wa madawati Changamoto nyingine ni mabadiliko ya mara kwa mara ya mitalaa yote haya yanachangia kurudisha nyuma maendeleo ya elimu.

Monday, May 14, 2012

NDEGE MPYA YA ATCL YATUA NCHINI

Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakishuka katika ndegempya aina ya Boeing 737-500 iliyokodishwa na shirika hilo yenye uwezo wa kubeba abiria 108. Ndege hiyo itaanza kuruka bada ya wiki moja.

Kaimu Mkurugenzi na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi akiongea na waandishi wa habari mara bada ya kuwasili kwa ndege mpya aina ya Boeing 737-500 iliyokodishwa na shirika hilo yenye uwezo wa kubeba abiria 108.

Wahudumu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) .

Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakikata keki kusherekea ujio wa ndege ndege mpya aina ya Boeing 737-500. Wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL ) Paul Chizi

MSAADA KWENYE TUTA.....

Huyu jamaa amekufa (Stephen Kanumba), nilitegemea matangazo yake yangesitishwa kwa kifo chake, je sheria na tamaduni vinasemaje? Tangazo hilo la Startimes kwenye kishikizo lipo kituo cha daladala mwenge.

From mdau

Sunday, May 13, 2012

OMG SIMBA IS OUT AISEE............!!


Imekuwa kama miujiza au tuseme ni mizimu imechukia mara baada ya kumsulubu mtani? Amini usiamini... Simba ya Tanzania imeondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa mikwaju ya penati 9-8.

Kipindi cha kwanza kilimalizika timu zote zikitoka sare ya bila kufungana.

Kipindi cha pili sekunde ya 23 walikuwa Al Ahly Shandy wenye ngekewa kuianza safari ya kupunguza magoli waliyochapwa wakiwa bongo nao bila ajizi ndani ya dakika 24 walikuwa tayari wamelipa deni kupitia makosa ya udhaifu wa ngome ya Simba, hadi dakika 90 zinamalizika simba ilikuwa imefungwa 3-0.

Ndipo time ya maamuzi mikwaju ya penati kwa mujibu wa kanuni za mashindano ikawadia.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam Simba ilishinda magoli 3-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ili kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho inayoandaliwa na Shirikisho la vyama vya mpira wa miguu Afrika (CAF) vizuri.

Hata hivyo imeshindwa kulinda ushindi wake mnono ilioupata jijini Dar es salaam na kukubali kipigo hicho kilichowasukumiza nje ya mashindano hayo.

MANCHESTER CITY MABINGWA ENGLAND

Mashabiki wa Manchester City wakishangilia ushindi Ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Queens Park Rangers 3-2,  jumapili ya May 13, 2012.
Manchester City ndiyo mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza ikiwa ni mara ya kwanza tangu 1968 baada ya ushindi wake wa leo kuichapa Queens Park Rangers 3-2 katika dimba la nyumbani Etihad Stadium.

Edin Dzeko alifunga bao la kusawazisha katika dakika za lala unono kabla ya Sergio Aguero kuifungia timu hiyo goli dakika nne za nyongeza lililowafanya kunyakua kombe hilo baada ya kulisotea kwa takribani miaka 40.
Sergio Aguero katikati ya ngome ya QPR
Both City and Manchester United finished with 89 points but Roberto Mancini's side were eight-goals superior after Sir Alex Ferguson's side defeated Sunderland 1-0.

City's long suffering fans invaded the pitch at full-time as a thrilling and unpredictable Premier League season reached its climax after the closest title race for over 20 years.

First place has fluctuated between the Manchester clubs all season with United top until the beginning of October before City went ahead until the start of March.

United then opened up an eight-point lead by Easter time but that evaporated after an erratic run and City went back to the summit on goal difference on April 30 when they beat United 1-0 at the Etihad.

HAPPY MOTHER'S DAY....!!!!!

Mama yangu mzazi Salome Charles akiwa na mjukuu wake.
Mamkubwa mama Mapesa akiwa na mjukuu wake na kwa chati mwingine 'smile to the fullest' laonekana usoni.
My lovery wife and our sons.
Pichani ni Hasheem Thabeet akifungwa kamba za viatu na mama yake mzazi, Rukia. Hapo ilikuwa Ikulu jijini Dar-es-salaam wakati Hasheem alipokwenda kumsalimia Rais Jakaya Kikwete 2009.
Marehemu mama mkwe wangu Evelyn
Marehemu Edna, mama wa jembe langu 'EduuuZ...'
HAPPY MOTHER'S DAY Kamwe thamani ya mama haitochuja, inyeshe mvua, liwake jua na hata siku isimame nani kama mama?

MALAWI MABINGWA KOMBE LA AFRICA NETIBOLI

Mabingwa wa michuano hiyo timu ya Malawi wakipiga picha pamoja na mgeni rasmi mama Asha Bilal.
 Timu ya Taifa Queen ikiwa katika picha ya pamoja na kombe lao.
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal wa nne kutoka kushoto na mama Tunu Pinda wanne kutoka kulia pamoja na wake wa viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya taifa ya Netiboli Taifa Queen mara baada ya kukabidhiwa kombe lao la ushindi wa pili katika michuano ya Afrika ya Netiboli, baada ya Malawi kuchukua ubingwa huo, fainali hizo zilifanyika jana kwenye uwanja wa Taifa wa ndani na kufuatiwa na hafla fupi nyumbani kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.

Hata hivyo fainali hizo zilichelewa kuanza kutokana na hali ya hewa ambapo muda mwingi mvua ilikuwa ikinyesha na kufanya waandaaji kuhamisha uwanja wa kuchezea mara kwa mara kutoka uwanja mkubwa wa Taifa na uwanja wa ndani Shukrani zimwendee mama Tunu Pinda kwani juhudi zake zilizozaa matunda na ni wazi kwamba hata wachezaji wa timu hiyo ya Taifa Queen wamefurahia sana michuano hii na wanajiona kwamba kweli walikuwa wakiwakilisha taifa, lakini pia pongezi ziwaendee watanzania wakiongozwa na mama Tunu Pinda pamoja na kamati yake, Hongera sana mama kwa kutoa zawadi nono kwa wachezaji.