ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 28, 2016

MAMBO MATANO MUHIMU YAKUZINGATIA MSIMU HUU WA SIKUKUU.

Mwezi huu wa kumi na mbili ni mwezi ambao una mapumziko na sikukuu nyingi. Ni mwezi ambao kunakuwa na sherehe mbalimbali na pia watu wengi wanakuwa kwenye mapumziko ya kazi.

Watu wengi wana taratibu mbalimbali unapofika mwezi huu wa mwisho wa mwaka. Wapo wanaofanya safari za mapumziko, wapo wanaorudi vijijini kwao na wapo wanaoendelea na shughuli zao kama kawaida TUNASEMA kufunga mahesabu..

Mwezi huu kunakuwa na matumizi makubwa sana ya fedha na hivyo wengi hujikuta katika wakati mgumu mwanzoni mwa mwaka. Kila mwanzo wa mwaka fedha inakuwa ngumu kwa watu wengi kutokana na matumizi mabovu mwishoni mwa mwaka. Watu wanakuwa wamefulia.

Ili kuboresha maisha yako na kujiondolea nyakati ngumu zinazoweza kutokea mwanzoni mwa mwaka kuna mambo mengi unaweza kufanya. Hapa nitazungumzia mambo matano muhimu ambayo ukiyafanya wakati huu wa mwisho wa mwaka utauanza mwaka mwingine ukiwa na ari na nguvu za kutosha.

1. Tafakari mwaka unaokwenda kuisha. Katika mwaka huu kuna mambo mengi uliyopanga kufanya. Yapo uliyofanikiwa kufanya na kuna ambayo uliyoshindwa kufanya. Pia kuna vikwazo mbalimbali ulivyokutana navyo. Hivyo ni vyema kuchukua muda na kutafakari mwaka ulivyokwenda kwa upande wako. (JIULIZE umefanya nini 2016?)

2. Tumia muda mwingi kukaa na familia na wale uwapendao. Kipindi hiki watoto wengi wapo likizo, na pia wazazi wengi wapo likizo pia. Huu ndio muda muhimu wa kuwa karibu na familia yako na kujifunza mengi ambayo unayakosa kutokana na majukumu ya kikazi. Tumia muda huu kuwa karibu na unaowapenda na wanaokupenda. Watembelee ndugu jamaa na marafiki na kubadilishana mambo mengi kuhusiana na maisha.

3. Pata muda wa kupumzika kweli. Japokuwa watu wengi wanakuwa na likizo kipindi hiki lakini wengi wanajikuta likizo zinaisha bila hata ya kupumzika. 

Wanajikuta wana majukumu mengi wakati huu wa likizo zaidi hata ya wakati wa kawaida wa kazi. Hata kama unavitu vingi vya kufanya bado unahitaji japo muda kidogo wa kupumzika. Kama shughuli zako hazikuruhusu kupumzika mwaka mzima basi unaweza kuwa na tatizo kubwa zaidi.

4. Kuwa mwangalifu katika matumizi. 
Kwa watu wengi wakati huu wanafanya matumizi yasiyo na mahesabu. Kwa sababu ni wakati wa sikukuu basi wananunua vitu ambavyo sio vya lazima, wanalewa sana na kufanya starehe nyingi. Kumbuka sikukuu sio mwisho wa dunia. Kuna maisha yataendelea baada ya msimu huu kupita, na kama usipokuwa makini utajuta sana mwanzoni mwa mwaka. Kuwa na bajeti ya matumizi, usisinunue kitu kwa sababu tu kila mtu ananunua, usinunue mti wa krismasi wa shilingi laki moja kwa sababu umeona unauzwa. Nunua vitu unavyohitaji na kulingana na uwezo wako.

5. Tumia muda huu wa mapumziko kuendeleza vipaji vyako ambavyo huvitumii wakati wa kazi. Una vipaji vingi ambavyo huwezi kuvionesha kwenye shughuli unazofanya. Wakati wa mapumziko unaweza kujifunza zaidi na kuendeleza kipaji chako. Inaweza kuwa uongozi, uandishi, uhamasishaji, uchoraji, uimbaji na mengine mengi. Pia tumia muda huu kujisomea vitabu mbalimbali vya kujifunza na kujihamasisha.

Tumia msimu huu wa sikukuu tofauti na ulivyotumia misimu mingine. Tumia wakati huu kuyaboresha maisha yako na kuwa na mpango mzuri na maisha yako. Usifanye mambo ambayo hayana manufaa kwenye maisha yako na ya wanaokuzunguka.
  Nakutakia kila la kheri kwenye mapumziko yako na heri ya mwaka mpya wa 2017.

WAMAREKANI WAANDAMANA DHIDI YA MSIMAMO WA TRUMP KUHUSU SILAHA ZA NYUKLIA.

Wananchi wa Marekani wamefanya maandamano katika mji wa New York wakikosoa wito uliotolewa hivi karibuni na Rais mteule wa nchi hiyo, Donald Trump wa kutaka kuimarishwa uwezo wa silaha za nyuklia wa nchi hiyo.
Wananchi hao wameandamana katika barabara za Midtown Manhattan na kisha kukita kambi nje ya jengo la Trump Tower wakikosoa wito huo wa Trump ambao wameutaja kuwa mashindano yasiyo na mantiki kati ya Marekani na Russia.
Baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji hao yalikuwa na ujumbe unaosema: "Hatutaki Nyuklia, Hatumtaki Trump!". Baadhi ya waandamanaji wameapa kutoondoka katika Medani ya Union jijini New York hadi pale Trump atakapobadili msimamo huo huku wakisisitiza kuwa, kuimarishwa uwezo wa silaha za nyuklia za Marekani ni jambo linalohatarisha mustakabali wa nchi hiyo.

Alkhamisi iliyopita, Trump alichapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa, nchi hiyo inapaswa kuimarisha zaidi uwezo wake wa silaha za nyuklia maadamu ulimwengu haujapata mwelekeo wa kimantiki kuhusu silaha za atomiki.
Donald Trump hakutoa maelezo zaidi katika uwanja huo lakini msemaji wake, Jason Miller alisema kuwa, rais huyo mteule wa Marekani alikuwa akiashiria vitisho vinavyohusiana na uzalishaji na uenezaji wa silaha za nyuklia na udharura wa kukabiliana na vitisho hivyo hususan vile vya makundi ya kigaidi katika maeneo yenye machafuko na "serikali au tawala za kigaidi."
Kwa sasa Marekani ina hifadhi ya vichwa 7000 vya silaha za nyuklia, ya pili duniani baada ya Russia ambayo ina mamia kadhaa ya vichwa hivyo zaidi ya Marekani.

Tuesday, December 27, 2016

KOCHA WA ZAMANI WA MAN UNITED ACHAGULIWA KUIFUNDISHA KRC GENK YA SAMATTA NA AKISHUHUDIA USHINDI

Klabu ya soka ya KRC Genk ya Ubelgiji, imemtangaza kocha wa zamani wa Manchester United Albert Stuivenberg kuwa kocha mpya atakayeifundisha timu hiyo.
Stuivenberg aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Louis Van Gaal kwenye timu ya United kwa misimu miwili kuanzia 2014 mpaka Juni 2016 na kufanikiwa kushinda kombe la FA msimu uliopita.
Albert Stuivenberg (kushoto) akiwa na Van Gaal pamoja na Ryan Giggs enzi za Manchester United.

Kocha huyo ambaye ni raia wa Uholanzi anachukuwa mikoba ya kuifundisha timu hiyo kutoka kwa Peter Maes ambaye ametimuliwa kutokana na kuwa na matokeo mabaya kwenye timu hiyo.

CHEKI VIDEO AKISHUHUDIA USHINDI SIKU YAKE YA UTAMBULISHO.

SAFARI YA MWISHO YA MPOKI BUKUKU : - NAPE, MBOWE WAONGOZA

 Wanahabari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku baada ya kutolewa heshima za mwisho katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es Salaam, tayari kulisafirishwa kwenda kwao Msalato Dodoma kwa mazishi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwaongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es Salaam. Mwili wa Mpoki ulisafirishwa kwenda kwao Msalato Dodoma kwa mazishi.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman  akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mpendwa wetu Mpoki Bukuku
 Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa akiwa ameshika shada la maua alipokuwa akiingiza kwenye gari lenye jeneza la mwili wa marehemu Mpoki Bukuku
 Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo ambaye pia ni Mmiliki wa Blog hii, Richard Mwaikenda akitoa salamu za rambirambi za Chama cha Mabloga Tanzania (TBN) wakati wa kuaga mwili wa mpendwa Mpoki Bukuku.
 Mwakilishi wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo  vya Habari Habari Tanzania (MOAT), Saed Kubenea akitoa salamu za rambirambi
 Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akitoa salamu za rambirambi
 Mwakilishi wa Chama cha Wapigapicha za Habar Tanzania (PPAT), Selemani Mpochi akitoa salamu za rambirambi. Mpoki alikuwa mwanachama wa chama hicho.
 ADMIN wa Group la WhatsApp la Tasnia, Thomson Kasenyenda akita salamu za rambirambi na kuahidi group hilo kuwasilisha mchango wao kwa kulipia ada za shule za watoto wa marehemu
 Mwenyekiti wa Chama cha Bongo Movie, Steven Nyerere akitoa salamu
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo na Burudani Tanzania (TASWA), Juma Pinto akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mpoki Bukuku.
 Benny Kisaka akitoa heshima za mwisho
 Mhariri Mtendaji wa The Guardian, Mgamba akitoa heshima za mwisho
 Mmiliki wa Blog ya Michuzi, Muhidini Issa Michuzi akitoa heshima za mwisho
 Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mpoki Bukuku

 Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete akitoka kutoa heshima za mwisho

 Mpigapicha wa The Guardian na Nipashe akisaidiwa baada ya kutoa heshima za mwisho
 Mpigapicha wa zamani wa Daily News, Athuman Khamisi akitoa heshima za mwisho
 Mtoto wa kike wa maraehemu Mpoki Bukuku akimvalisha Rozali wakati wa kuaga mwili wa babake
 Mjane wa marehemu Lillian  akiubusu mwili wa mumewe
 Mtoto wa kiume wa marehemu Mpoki Bukuku, Junior akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa babake

Jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu Mpoki Bukuku likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Msalato Dodoma kwa mazishi.

IDADI YA WATU WASIO NA MAKAZI WALA NYUMBA YAVUNJA REKODI MAREKANI.


Ripoti iliyotolewa na Muungano wa Taifa kwa Ajili ya Kukomesha Hali ya Kutokuwa na Makazi nchini Marekani (National Alliance to End Homelessness) inaonesha kuwa, idadi ya watu wasio na makazi nchini humo imeongezeka kwa kiasi ambacho hakijawahi kushuhudiwa.

Ripoti ya muungano huo iliyotolewa jana Jumapili imesema kuwa, kila usiku Wamarekani zaidi ya laki tano na 60 elfu hulala nje mitaani. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, idadi ya Wamarekani wanaolala nje na wasio na makazi katika mji wa New York imefikia kiwango cha juu sana baada ya kile kilichoshuhudiwa katika kipindi cha mdororo mkubwa wa uchumi wa mwaka 1930 nchini Marekani.



Maelfu ya Wamarekani wanalala mitaani
Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa, Wamarekani 17 kati ya kila elfu kumi hawana nyumba wala makazi na wanalazimika kulala mitaani.

Takwimu hizo zinasema kuwa, wastani wa watu wasio na nyumba wala makazi nchini Marekani ni zaidi ya watu laki tano na kwamba laki 1 na elfu 25 kati yao ni watoto wadogo.

Takwimu zinaonesha kuwa mji wa Los Angeles ndio wenye idadi kubwa zaidi ya watu wasio na makazi nchini Marekani na kwamba karibu watu wote hao wanaishi mitaani.  

WANAWAKE NA WATOTO NI WAHANGA WA VISA VYA UNYANYASAJI DUNIANI.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa wanawake na watoto ni wahanga wakubwa wa visa vya unyanyasaji na magendo ya binadamu duniani.
Ofisi ya Kupambana na Jinai na Madawa ya Kulevya ya Umoja wa Mataifa (ONUDC) imetangaza katika ripoti yake ya kila mwaka kuhusu mwaka huu wa 2016 kuwa, asilimia 71 ya wahanga wa magendo ya binadamu na vitendo vya unyanyasaji ni wanawake na watoto; ambapo theluthi moja ya idadi hiyo inaundwa na watoto. Yury Fedotov Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC amewasilisha ripoti hiyo ya kila mwaka ya Ofisi ya Kupambana na Jinai na Mihadarati ya Umoja wa Mataifa na kueleza kuwa, utumwa wa ngono na kazi za lazima ni kesi walizodhibitisha katika ripoti hiyo.
Mtoto ambaye amekuwa akitumiwa kama askari jeshi katika mizozo ya ndani barani Afrika 
Hata hivyo amesema kuwa wanawake na mabinti ni wahanga pia wa  kuolewa kwa lazima, ufisadi na kuporomoka kimaadili.

Ripoti hiyo ya kila mwaka ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Jinai na Madawa ya Kulevya imeongeza kuwa wanawake na mabinti kwa ujumla huwa wahanga wa utumwa wa ngono  huku wanaume na wavulana wakitumiwa kama wapagazi katika michimbo ya madini, na askari jeshi  katika mizozo ya ndani. 


 Ripoti ya UNODC imeongeza kuwa, jumla ya asilimia 28 ya wahanga duniani ni watoto.


SABODO AMSHAURI RAIS MAGUFULI AZIDI KUPUNGUZA BARAZA LA MAWAZIRI

 Mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo akizungumza nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki, ambapo alimtaka Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Rais John Magufuli azidi kupunguza Baraza la Mawaziri kufikia 15 na Kamati Kuu 15 pamoja na Halmashauri Kuu wajumbe 55. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


MFANYABIASHARA maarufu nchini, Jaffar Sabodo, amemshauri Rais John Magufuli kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri, akisema hali hiyo itamsaidia kuleta tija zaidi katika utendaji wake.

Aidha, Sabodo amemshauri Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupunguza idadi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na JAMBO LEO nyumbani kwake Dar es Salaam, Sabodo alisema hatua hiyo itasaidia Serikali kutekeleza falsafa yake ya kubana matumizi.

“Kupungua kwa ukubwa wa Baraza la Mawaziri kutajenga uwajibikaji zaidi kwa mawaziri, lakini pia kubana matumizi ya Serikali kuhudumia baraza kubwa la mawaziri pia kusaidia kujenga mfumo imara zaidi wa utawala na itakuwa rahisi kudhibiti siri za Serikali,” alisema Sabodo na kuongeza:

“Hata ukubwa wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu za CCM nao ukipungua utaiimarisha zaidi CCM, kwani viongozi wake watakuwa na nguvu zaidi, lakini pia matumizi yatapungua na mambo ya chama hayatavujishwa kirahisi.”


Alipoulizwa kuhusu idadi anayopendekeza iwe kwa vyombo hivyo, Sabodo ambaye amewahi kuwa mfadhili wa CCM na Chadema kwa nyakati tofauti alisema: “Ili kulinda zaidi maadili ya CCM yawe kama alivyoacha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyeiasisi, kwa mawazo yangu Halmashauri Kuu ingekuwa na wajumbe wasiozidi 55 na Kamati Kuu wawepo wajumbe wasiozidi 15.”

Kuhusu Baraza la Mawaziri Sabodo alisema linapaswa kupungua kutoka idadi ya sasa hadi kufikia mawaziri wasiozidi 15. “Cabinet’ baraza liwe dogo, kuna wizara zinaweza kufutwa, ili kuleta tija zaidi. Hili linawezekana,” alisema Sabodo.

Ushauri huo wa Sabodo umekuja wakati hivi karibuni CCM ilitangaza mabadiliko na kupunguza idadi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka 388 hadi 158 huku wajumbe wa Kamati Kuu ikipunguzwa kutoka 34 hadi 24.

Kwa upande wa mawaziri, Baraza la Mawaziri la Rais Magufuli lina mawaziri kamili 20 pamoja na Waziri Mkuu, likiwa na naibu mawaziri 16.

Akizungumzia uamuzi wa Rais Magufuli kuhamia Dodoma, Sabodo alisema ameonesha uthubutu ulioshindikana kwa zaidi ya miaka 45.

Alisema anakumbuka uamuzi wa kuhamia Dodoma ulifikiwa na Bunge enzi za utawala wa hayati Mwalimu Julius Nyerere aliyeshindwa kuufanikisha kutokana na sababu mbalimbali za msingi, lakini waliofuata katika uongozi hakuna aliyeonyesha uthubutu kama wa Rais magufuli.

Sabodo alisema hatua hiyo ya kuhamia Dodoma ikifanikiwa inaweza kusaidia hata rushwa na ubadhirifu kupungua kwani baadhi ya mambo yatashindikana kufanyika Dar es Salaam litakalobaki kama jiji la kibiashara hivyo kuwalazimu wahusika kwenda makao makuu ya Serikali.

Monday, December 26, 2016

MZEE WA UPAKO AFUKUZA WAANDISHI.

MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo maarufu 'Mzee wa Upako, aliwagomea waandishi wa habari kusikiliza hotuba yake ya ibada na kutuma wasaidizi wake wawaondoe waandishi hao.
“Samahani tunaomba muondoke kwani Mchungaji amesema hataki kumuona mwandishi hivyo tunaomba muende kwenye makanisa mengine,” alisema msaidizi huyo na kuhakikisha waandishi wote wanaondoka eneo hilo majira ya saa sita kasoro mchana.

Lusekelo maarufu Mzee wa Upako hivi karibuni amekuwa akirushiana maneno na baadhi ya waandishi wa habari baada ya kuandikwa akituhumiwa kuwa mlevi na kutukana hadharani.

Desemba 25 ya kila mwaka, waumini wa dini ya Kikristo nchini huungana na wenzao duniani kuadhimisha sherehe za kuzaliwa kwa Bwana wao Yesu Kristo yapata miaka 2000 iliyopita.

Wakati huohuo waumini wa dini ya Kikristo nchini wametakiwa kudumisha upendo, utii na unyenyekevu ili kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bwana na Mwokozi wao Yesu Kristo ikiwa ni pamoja na kuliombea amani taifa lao la Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ibada ya mkesha wa sikukuu hiyo, Dk Alex Malasusa, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, aliwataka waumini wa kanisa hilo, kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa amani na upendo kwa wenzao.

Alisema siku ya Krismasi ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwana wa Mungu Yesu Kristo ambaye kutokana na upendo wake, aliwaunganisha watu na Mwenyezi Mungu.

“Tuuenzi upendo wake, lakini kubwa zaidi tukumbuke kuwa amani ndio msingi wa sikukuu hii. Hata alipokuja Yesu maneno yake ya kwanza yalikuwa ni amani,” alisisitiza. Askofu Malasusa, aliwataka wananchi katika kudumisha upendo huo, waliombee taifa pamoja na viongozi wake ili amani iliyopo iendelee kudumu.

“Ndio maana leo katika ibada yetu ya mkesha wa Krismasi tumeamua kupeana zawadi ikiwa ni ishara ya kuoneshana upendo na kudumisha amani miongoni mwetu,” alisema.

Mara baada ya ibada hiyo, waumini wa kanisa hilo, walibadilishana zawadi ambayo kila mtu alikuja nayo na kumpatia mwenzake huku Askofu Malasusa na viongozi wengine wa Kanisa hilo nao wakigawa zawadi zao kwa waumini hao.

Sunday, December 25, 2016

YESU ALIZALIWA WAKATI GANI?


Maoni ya Biblia
Yesu Alizaliwa Wakati Gani?
“TAREHE hususa ambayo Kristo alizaliwa haijulikani,” inasema Encyclopedia of Early Christianity. Hata hivyo, mamilioni ya watu wanaodai kuwa Wakristo ulimwenguni pote husherehekea kuzaliwa kwa Yesu Desemba (Mwezi wa 12) 25. Lakini tarehe hiyo haionekani mahali popote katika Biblia. Je, kweli Yesu alizaliwa Desemba?
Ingawa Biblia haitupi tarehe hususa ya kuzaliwa kwa Yesu, inatoa uthibitisho wa kwamba hakuzaliwa Desemba. Mbali na Biblia kuna uthibitisho mwingine unaoweza kutusaidia kujua kwa nini Desemba 25 ilichukuliwa kuwa tarehe ya kusherehekea kuzaliwa kwake.
Kwa Nini Hakuzaliwa Desemba?
Yesu alizaliwa katika jiji la Bethlehemu huko Yudea. Injili ya Luka inaripoti hivi: “Katika nchi hiyo kulikuwako pia wachungaji wakiishi nje, wakichunga makundi yao usiku.” (Luka 2:4-8) Hilo lilikuwa jambo la kawaida. “Kwa miezi mingi mifugo ilikuwa katika maeneo yaliyo wazi,” kinasema kitabu Daily Life in the Time of Jesus. Lakini je, wachungaji wangekuwa nje na mifugo yao katika usiku wenye baridi wa Desemba? Kitabu hicho kinasema: “Katika majira ya baridi kali walikuwa ndani ya nyumba; na hilo peke yake linafanya tarehe ya Krismasi, katika majira ya baridi kali, kuwa si sahihi kwa sababu Injili inasema wachungaji walikuwa mashambani.”
Mkataa huo unapatana na habari nyingine katika Injili ya Luka: “Katika siku hizo Kaisari Augusto alitoa amri kwamba dunia yote inayokaliwa iandikishwe; (uandikisho huu wa kwanza ulitendeka wakati Kirenio alipokuwa gavana wa Siria;) na watu wote wakaanza kusafiri kwenda kuandikishwa, kila mmoja kwenye jiji lake mwenyewe.”—Luka 2:1-3.
Huenda Augusto aliamuru uandikisho huo ili atumie habari hiyo kuhusiana na kutoza ushuru na kuandikisha watu jeshini. Ili atii amri hiyo, Maria, aliandamana na mume wake, Yosefu, katika safari ya kilomita 150 hivi kutoka Nazareti kwenda Bethlehemu ingawa alikuwa karibu kuzaa. Sasa hebu fikiria kuhusu jambo hilo. Je, inapatana na akili kwamba Augusto, mtawala ambaye hakujihusisha sana na serikali za wilaya, angewaamuru watu ambao walikuwa tayari kuzusha ghasia dhidi ya utawala wa Waroma wafunge safari hiyo ndefu katika majira ya baridi kali?
Ni muhimu kujua kwamba wanahistoria na wasomi wengi wa Biblia wanapinga kwamba Yesu alizaliwa Desemba 25. Bila shaka, utapata habari hiyo katika ensaiklopedia mbalimbali. Our Sunday Visitor’s Catholic Encyclopedia inasema: “Watu wengi wanakubaliana kwamba Yesu hakuzaliwa Desemba 25.”
Kwa Nini Walichagua Desemba 25?
Mamia ya miaka baada ya kifo cha Yesu, Desemba 25 ilichaguliwa kuwa tarehe ya kuzaliwa kwake. Kwa nini? Wanahistoria wengi wanaamini kwamba wakati ambao sasa Krismasi husherehekewa ulikuwa wakati wa sherehe za kipagani.
Kwa mfano, Encyclopædia Britannica inasema: “Ufafanuzi mmoja ulioenea wa chanzo cha tarehe hii ni kwamba sikukuu ya dies solis invicti nati (‘siku ya kuzaliwa kwa jua lisiloshindwa’) iliyosherehekewa Desemba 25, ilifanywa kuwa ya Kikristo. Hiyo ilikuwa sikukuu maarufu ya Milki ya Roma iliyosherehekewa wakati jua linapochomoza katika majira ya baridi kali kama ishara ya mwisho wa majira hayo na mwanzo wa majira ya kupukutika na kiangazi.”
Kitabu The Encyclopedia Americana kinatuambia hivi: “Sababu ya kutenga Desemba 25 kuwa Krismasi haijulikani, lakini inaaminiwa kwamba siku hiyo ilichaguliwa ili ilingane na sherehe ya kipagani iliyofanyika jua lilipochomoza katika majira ya baridi kali, wakati mchana ulianza kuwa mrefu, ili kusherehekea ‘kuzaliwa tena kwa jua.’ . . . Satanalia ya Kiroma (sherehe ya Saturn, mungu wa kilimo, na nguvu mpya za jua), pia ilifanyika wakati huo.” Kwa kawaida, sherehe hizo zilitia ndani mwenendo mpotovu kingono ambapo watu walisherehekea bila kujizuia na kwa kelele nyingi sana. Tabia hizohizo huonekana katika sherehe nyingi za Krismasi leo.
Jinsi ya Kumheshimu Kristo
Watu fulani wanahisi kwamba hata ingawa hatujui tarehe hususa, ni lazima Wakristo washerehekee kuzaliwa kwa Yesu. Kwa maoni yao, sherehe hiyo inapofanywa kwa njia inayofaa ni njia nzuri ya kumheshimu Kristo.
Kwa kweli, kuzaliwa kwa Yesu ni tukio muhimu katika Biblia. Biblia inasema kwamba Yesu alipozaliwa, umati wa malaika ulitokea ghafula na kumsifu Mungu kwa shangwe wakisema: “Utukufu katika vilele vilivyo juu kwa Mungu, na juu ya dunia amani kati ya watu wa nia njema.” (Luka 2:13, 14) Hata hivyo, ni muhimu kutambua kwamba hakuna mahali popote katika Biblia ambapo inasemekana kwamba siku ya kuzaliwa kwa Yesu inapaswa kusherehekewa. Kinyume na hilo, kuna amri hususa ya kuadhimisha kifo chake. Mashahidi wa Yehova hufanya hivyo mara moja kwa mwaka. (Luka 22:19) Hiyo ni njia moja ya kumheshimu Yesu.
Usiku wake wa mwisho akiwa mwanadamu, Yesu alisema: “Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mnafanya ninalowaamuru ninyi.” (Yohana 15:14) Pia alisema: “Ikiwa mnanipenda, mtazishika amri zangu.” (Yohana 14:15) Ni wazi kwamba hakuna njia bora zaidi ya kumheshimu Yesu Kristo kuliko kujifunza na kufuata mafundisho yake.
JE, UMEJIULIZA HIVI?
▪ Kwa nini haiwezekani kuwa Yesu alizaliwa Desemba?—Luka 2:1-8.
▪ Ni nini muhimu kuliko siku ambayo mtu alizaliwa?—Mhubiri 7:1.
▪ Ni njia gani bora zaidi ya kumheshimu Yesu?—Yohana 14:15.
[Picha katika ukurasa wa 11]
Biblia inatoa uthibitisho wa kwamba Yesu hakuzaliwa Desemba
[Picha katika ukurasa wa 10]
Je, wachungaji wangekuwa nje na mifugo yao usiku katika theluji?
[Hisani]
Todd Bolen/Bible Places.com

91 WAHOFIWA KUFA BAADA YA NDEGE YA KJESHI YA RUSIA KUANGUA BAHARINI

Makumi ya watu wanahofiwa kupoteza maisha baada ya ndege ya kijeshi ya Russia kuanguka katika Bahari Nyeusi, muda mfupi baada ya kutoweka kwenye rada.
Wizara ya Ulinzi ya Russia imethibitisha habari hizo na kusema kuwa, ndege hiyo ya kijeshi yenye nambari ya usajili Tu-154 ilikuwa imebeba abiria 83 na wahudumu wanane.
Habari zinasema kuwa, ndege hiyo ilitoweka kwenye rada muda mfupi baada ya kupaa angani, ikitokea uwanja mmoja wa ndege katika mji wa pwani wa Sochi.
Mabaki ya ndege ya Russia iliyoanguka miezi 11 iliyopita.

EXLUSIVE INTERVIEW: MBATIA HERI KIFO KULIKO MAISHA YA TABU.

Mbunge wa jimbo la Vunjo na Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi,James Mbatia amesema Tanzania inahitaji kuwekeza zaidi katika elimu ili kuinusuru sekta ya afya kwani amedai kuwa Watanzania wengi ni wagonjwa lakini hawajijui.

NINI MAANA YA KRISMASI FUATILIA MADA HII

Fuatilia mazungumzo kuhusu maana ya Krismasi na umuhimu wa kusherekea siku kuu ya Krismasi.

MAGAZETI YA LEO:- UVCCM WAMKAANGA DC BUKOA MJINI, JPM AUMA APULIZA, KINACHOMPATA LOWASSA MATUMAINI 2020


CH 10: UVCCM wamkaanga DC Bukoba mjini, JPM auma, apuliza,kinachompa Lowassa matumaini 2020,Lowassa alivyowapa ulaji Nape, Makonda,Habari njema sindano ya kung’atwa nyoka. 

TBC: Majambazi yavamia  yaua mgodini , 80 mbaroni kwa wizi wa mamilioni ya TASAF,  Magufuli kusali Krismasi Singida, Polepole afunguka, Polisi waingia lawamani. Pata dondoo za magazeti ya leo hapa.