ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 28, 2016

WAMAREKANI WAANDAMANA DHIDI YA MSIMAMO WA TRUMP KUHUSU SILAHA ZA NYUKLIA.

Wananchi wa Marekani wamefanya maandamano katika mji wa New York wakikosoa wito uliotolewa hivi karibuni na Rais mteule wa nchi hiyo, Donald Trump wa kutaka kuimarishwa uwezo wa silaha za nyuklia wa nchi hiyo.
Wananchi hao wameandamana katika barabara za Midtown Manhattan na kisha kukita kambi nje ya jengo la Trump Tower wakikosoa wito huo wa Trump ambao wameutaja kuwa mashindano yasiyo na mantiki kati ya Marekani na Russia.
Baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji hao yalikuwa na ujumbe unaosema: "Hatutaki Nyuklia, Hatumtaki Trump!". Baadhi ya waandamanaji wameapa kutoondoka katika Medani ya Union jijini New York hadi pale Trump atakapobadili msimamo huo huku wakisisitiza kuwa, kuimarishwa uwezo wa silaha za nyuklia za Marekani ni jambo linalohatarisha mustakabali wa nchi hiyo.

Alkhamisi iliyopita, Trump alichapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa, nchi hiyo inapaswa kuimarisha zaidi uwezo wake wa silaha za nyuklia maadamu ulimwengu haujapata mwelekeo wa kimantiki kuhusu silaha za atomiki.
Donald Trump hakutoa maelezo zaidi katika uwanja huo lakini msemaji wake, Jason Miller alisema kuwa, rais huyo mteule wa Marekani alikuwa akiashiria vitisho vinavyohusiana na uzalishaji na uenezaji wa silaha za nyuklia na udharura wa kukabiliana na vitisho hivyo hususan vile vya makundi ya kigaidi katika maeneo yenye machafuko na "serikali au tawala za kigaidi."
Kwa sasa Marekani ina hifadhi ya vichwa 7000 vya silaha za nyuklia, ya pili duniani baada ya Russia ambayo ina mamia kadhaa ya vichwa hivyo zaidi ya Marekani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.