Makumi ya watu wanahofiwa kupoteza maisha baada ya ndege ya kijeshi ya Russia kuanguka katika Bahari Nyeusi, muda mfupi baada ya kutoweka kwenye rada.
Wizara ya Ulinzi ya Russia imethibitisha habari hizo na kusema kuwa, ndege hiyo ya kijeshi yenye nambari ya usajili Tu-154 ilikuwa imebeba abiria 83 na wahudumu wanane.
Habari zinasema kuwa, ndege hiyo ilitoweka kwenye rada muda mfupi baada ya kupaa angani, ikitokea uwanja mmoja wa ndege katika mji wa pwani wa Sochi.
Mabaki ya ndege ya Russia iliyoanguka miezi 11 iliyopita. |
Habari zaidi zinasema kuwa, ndege hiyo iliyokuwa imebeba wanajeshi, waandishi wa habari na wanamuziki, ilikuwa ikielekea katika mkoa wa Latakia nchini Syria.
Russia ambayo ina vituo viwili vya jeshi la anga nchini Syria, imekuwa ikifanya mashambulizi dhidi ya magaidi katika nchi hiyo ya Kiarabu, kutokana na ombi la serikali ya Damascus.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.