Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa wanawake na watoto ni wahanga wakubwa wa visa vya unyanyasaji na magendo ya binadamu duniani.
Ofisi ya Kupambana na Jinai na Madawa ya Kulevya ya Umoja wa Mataifa (ONUDC) imetangaza katika ripoti yake ya kila mwaka kuhusu mwaka huu wa 2016 kuwa, asilimia 71 ya wahanga wa magendo ya binadamu na vitendo vya unyanyasaji ni wanawake na watoto; ambapo theluthi moja ya idadi hiyo inaundwa na watoto. Yury Fedotov Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC amewasilisha ripoti hiyo ya kila mwaka ya Ofisi ya Kupambana na Jinai na Mihadarati ya Umoja wa Mataifa na kueleza kuwa, utumwa wa ngono na kazi za lazima ni kesi walizodhibitisha katika ripoti hiyo.
Mtoto ambaye amekuwa akitumiwa kama askari jeshi katika mizozo ya ndani barani Afrika |
Ripoti hiyo ya kila mwaka ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Jinai na Madawa ya Kulevya imeongeza kuwa wanawake na mabinti kwa ujumla huwa wahanga wa utumwa wa ngono huku wanaume na wavulana wakitumiwa kama wapagazi katika michimbo ya madini, na askari jeshi katika mizozo ya ndani.
Ripoti ya UNODC imeongeza kuwa, jumla ya asilimia 28 ya wahanga duniani ni watoto.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.