ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 4, 2013

PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA MKUTANO WA 10 WA WADAU WA SEKTA NDOGO YA ZAO LA PAMBA

Waziri mkuu Mizengo Pinda (katikati), wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Dr. Festus Limbu (MB), Naibu waziri wa Chakula na Ushirika Adam Malima (MB) na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dkt. Antony Dialo, Kaimu mkuu wa mkoa Baraka Konisaga (DC Nyamagana). Nyuma ni kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza.

Mmoja wa wanachama wa TACOGA ambaye ni mkulima wa zao la pamba akichangia hoja.

Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi Mhe. John Cheyo akichangia hoja katika kikao hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha benki kuu (BOT) Capripoint jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa TCA na Mnunuzi wa Pamba Christopher Mwita Gachuma (MNEC - Tarime) akiwa na wajumbe wengine.

Sehemu ya wajumbe kwenye mkutano huo.

Wajumbe mkutanoni hapa.

Mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi Mhe. John Magale Shibuda akichukua nondo zilizokuwa zikitolewa na wadau wa pamba ndani ya mkutano huo.

Baadhi ya wakuu wa wilaya nao walikuwa ni sehemu ya wajumbe wa mkutano huu.

Kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Paschal Mabiti, Joel Mkaya Bendera (Morogoro), na wengine wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya waziri mkuu.

Picha ya pamoja waziri mkuu Mizengo Pinda (katikati) na kushoto kwa waziri mkuu ni Naibu waziri wa wizara ya Chakula na ushirika Adam Malima (MB), waziri wa Nchi utumishi Celina Kombani (MB) na Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Kassim Majaliwa. Kulia kwa Waziri mkuu ni Kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Baraka Konisaga (DC Nyamagana), Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba nchini Dr. Festus Limbu (MB) na Naibu waziri wa wizara ya Uchukuzi Dr. Charles Tizeba (MB)  wakiwa na wakuu wa Mikoa na Wilaya kutoka mikoa 15 inayolima zao la pamba nchini.

Picha ya pamoja waziri mkuu Mizengo Pinda (katikati) na kushoto kwa waziri mkuu ni Naibu waziri wa wizara ya Chakula na ushirika Adam Malima (MB), waziri wa Nchi utumishi Celina Kombani (MB) na Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dkt. Anthony Dialo. Kulia kwa Waziri mkuu ni Kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Baraka Konisaga (DC Nyamagana), Mwenyekiti wa Bod ni ya Pamba nchini Dr. Festus Limbu (MB) na Naibu waziri wa wizara ya Uchukuzi Dr. Charles Tizeba (MB)  wakiwa na Wabunge na Wenyeviti wa Halmashauri. 

MITINDO YA MIKAO NA MASTYLE ILE NKABAAaaaa!!!

'Dabliyu thing' (W) ya kundi la Bombeso.

Slide ya Bombeso.

Hapo vipi na K mgeuko?

Yep....

Peace

Ni kundi zima la Bombeso moja wa washindi wa shindano la kwanza la Dance la Fiesta ndani ya tamasha kubwa Tanzania  Fiesta. 

Kundi la Jacson 5 la jijini Mwanza.

Pyuuuu...!!

Wednesday, July 3, 2013

BRAND NEW SONG: MO THAN LUV by METTY

Kuwa wa kwanza kusikiliza wimbo mpya toka kwa Metty a.k.a Magese ambao umetoka leo hii. "Since 1998 niko kwa hili gem nimerudi kwa miguu minne"

  #hi wave inadownlika tu hapo chini
enter-tz Unique shared this file from Dropbox:

MOROGORO YAISHINDILIA TEMEKE 5-2 MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS

Timu za Airtel Rising Stars zikiingia kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam tayari kwa ufunguzi rasmi wa ARS ngazi ya Taifa jana Jumanne Julai 2, 2013..
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano – Mallya akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini  Dar es Salaam jana Jumanne Julai 2, 2013. 
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa uliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini  Dar es Salaam jana Jumanne Julai 2, 2013.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Kassim Majaliwa akikagua timu za mikoa ya Mwanza na Ilala ambazo zilichuana kwenye hafla ya kufungua rasmi mashindano ya Taifa ya Airtel Rising Stars kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini  Dar es Salaam jana Jumanne Julai 2, 2013. Mwanza ilishinda 3-1.
Mashabiki wa soka wakishuhudia vipaji vya soka wakati wa mechi ya Airtel Rising Stars kati ya Mwanza na Ilala kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini  Dar es Salaam Jumanne Julai 2, 2013. Mwanza ilishinda 3-1.

Morogoro yailaza Temeke 5-2 Airtel Rising Stars
    Ilala wasichana waibamiza Ruvuma 9-0


Timu ya Morogoro wavulana leo Jumatano Julai 3, imeifunga timu ya Temeke 5-2 katika fainali za Taifza za Airtel Rising Stars zinazoendelea kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.

Morogoro waliutawala mchezo na kufanikiwa kupata magoli kupitia kwa mshambuliaji wa machachali Optatus Lupekenya ambaye alifunga magoli matatu peke yake yaani ‘hat trick’ katika dakika za 27 67 na 87.


Magoli mengine ya Morogoro yalifungwa Salum Mohamed dakika ya 72 na Evance Noshan dakika ya 80 wakati magoli ya Temeke yalifungwa na Mohamed Simba dakika ya 10 na Rajab Jumanne dakika ya 83.

Katika mchezo uliochezwa mapema asubuhi timu ya Ilala wasichana ilifanya mauaji ya kutisha baada ya kuifunga bila huruma timu ya Ruvuma 9-0 katika mchezo wa upande mmoja wa fainali za Taifa za Airtel Rising Stars. Mchezo huo ulionyesha wazi ya kuwa Ruvuka wanatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kuinua kiwango chao cha soka.

Ilala walifunga magoli yao kupitia kwa Amina Ally (dakika ya 3, 28 na 51), Donisia Daniel (dakika ya 20 na 45), Zuwena Aziz (dakika ya 23 na 35), Madeline Sylvester (dakika ya 8) na Fatuma Bahau (dakika ya 12).

Katika mchezo uliochezwa Jumanne jioni katika uwanja huo huo, timu ya kombaini ya Mwanza (wavulana) ilitoa onyo kwa timu zinazoshiriki michuano hiyo baada ya kuifunga timu ngumu ya Ilala 3-1.

Huo ulikuwa mchezo rasmi wa ufunguzi wa Airtel Rising Stars Taifa 2013 ambapo mgeni rasmi Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Kassim Majaliwa aliwataka vijana kuonyesha vipaji vyao.

“Katika dunia ya leo mpira wa miguu ni moja ya vyanzo vya ajira vya kutumainiwa kwa vijana”, alisema Majaliwa na kuwahamasisha vijana hao kucheza kwa kujituma na kutumia mashindano ya Airtel Rising Stars kama fursa ya kuonyesha umahiri wao wa kusakata kabumbu. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano alisisitiza nia thabiti ya kampuni yake kuendeleza kusaidia programu hii ya vijana.

Mcheo kati ya Mwanza na Ilala ulikuwa wa kuvutia huku timu zote zikionyesha kiwango kizuri kwa kugongeana pasi za uhakika. Mwanza walifanikiwa kupata goli la kwanza dakika ya saba kupitia kwa Nassor ambaye aliwapita walinzi wa Ilala na kutia mpira wavuni. Goli hilo lilidumu hadi mapumziko.

Ilala walianza kipindi cha pili kwa nguvu na kupata goli la kusawazisha dakika ya 50 kupitia mpira wa adhabu uliopigwa na Omary Hassan baada ya walinzi wa Mwanza kufanya makosa nje kidogo ya eneo la hatari. Mshambuliaji Athanas Adam aliifungia Mwanza goli la pili dakika ya 69 na Kelvin Ntalale kugongelea msumari wa mwisho dakika
mbili kabla ya mchezo kumalizika.

TANROAD YACHOMA MABANDA YA WAFANYABIASHARA WAKAIDI MWANZA

TANROAD mkoa wa Mwanza inaendesha zoezi la kuwaondosha wafanyabiashara ndogondogo waliokiuka utaratibu uliowekwa wa kuwataka kutofanya biashara zao kandokando mwa barabara za Mwanza - Musoma na Mwanza - Shinyanga hivi ndivyo zoezi hilo lilivyofanyika huku ulinzi mkali ukihusishwa. 

Kuvamia kwa wafanyabiashara katika maeneo haya ya miliki ya barabara kunasababisha ajali, kuwepo na ufinyu wa watumiaji wa barabara wakiwemo watembea kwa miguu.

Kutokana na kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha mkoa wa Mwanza kilichokaa na kukubaliana na ombi la TANROAD la kuwaondoa wafanyabiashara hao waliojikita ndani ya hifadhi ya barabara.

Gari la TANROAD na vifaa vyake kikazi zaidi.

Zoezi hilo linafanywa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Tokea mwezi wa nne mwaka huu (2013) amri  na muda maalum uliwekwa kwa wafanyabiashara wote waliovamia hifadhi za barabara hizo kuondoka mara moja hivyo zoezi la sasa linawahusu wale waliokaidi. 

RED CAPET YA MISS LAKE ZONE 2013

Colours
Utaifa zaidi.
Dadaz
Gentle
Stylish.
Protocal 
Good.
Chick as Gaga.
Yeah.
Cinderella.
Talk. 
Wow.
Junk Yunk.
Ladies.
Flowers.
Supa dupaz.
PICHA KWA HISANI YA TROPICAL MEDIA

AKILI MATOPEeee....!!?

Haijalishi unarasilimali kiasi gani, kama hujui jinsi ya kuzitumia, siku zote hazitokutosha.

Tuesday, July 2, 2013

ELIMU YA MAAFA YATOLEWA KWA WADAU WA KAMATI MBALIMBALI ZA ULINZI NA USALAMA WILAYA ZA MKOA WA MWANZA

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akifungua mafunzo ya elimu kuhusu maafa kwa wadau wa kamati za maafa wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza, hii leo yaliyofanyika katika ukumbi wa hotel JB Belmont jijini Mwanza.

Washiriki wa kamati za ulinzi na usalama ndani ya semina ya mafunzo hayo kwenye kona kabisa (kulia) anaonekana Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Mwanza MWAUWASA. 

Suala la wananchi kupuuza taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa zinazotolewa na vituo husika ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili idara ya maafa kama alivyoainisha Mkurugenzi wa Idara hiyo Taifa Luteni Jenerali Mstaafu Slyvester Lioba.

Sehemu ya washiriki.

Tayari mpaka sasa Idara ya maafa Taifa imetoa mafunzo kama haya kwa mikoa yote nchini ikiwa imesalia mikoa saba tu kukamilisha zoezi la nchi nzima.

Kutoka kushoto ni Katibu wa Bakwata mkoa, anayefuata ni Shekhe wa Mkoa na mdau mwingine.

Nao washiriki toka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza wamesisitizwa kuzingatia mafunzo yaliyotolewa na kuyatumia vyema ili kujenga uwezo kwa kamati zao kukabili kwa mafanikio maafa yanapojitokeza sehemu walizopo.

Wakuu na mazungumzo ya hapana pale...

Picha ya pamoja ya viongozi na washiriki.