ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 2, 2013

ELIMU YA MAAFA YATOLEWA KWA WADAU WA KAMATI MBALIMBALI ZA ULINZI NA USALAMA WILAYA ZA MKOA WA MWANZA

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akifungua mafunzo ya elimu kuhusu maafa kwa wadau wa kamati za maafa wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza, hii leo yaliyofanyika katika ukumbi wa hotel JB Belmont jijini Mwanza.

Washiriki wa kamati za ulinzi na usalama ndani ya semina ya mafunzo hayo kwenye kona kabisa (kulia) anaonekana Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Mwanza MWAUWASA. 

Suala la wananchi kupuuza taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa zinazotolewa na vituo husika ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili idara ya maafa kama alivyoainisha Mkurugenzi wa Idara hiyo Taifa Luteni Jenerali Mstaafu Slyvester Lioba.

Sehemu ya washiriki.

Tayari mpaka sasa Idara ya maafa Taifa imetoa mafunzo kama haya kwa mikoa yote nchini ikiwa imesalia mikoa saba tu kukamilisha zoezi la nchi nzima.

Kutoka kushoto ni Katibu wa Bakwata mkoa, anayefuata ni Shekhe wa Mkoa na mdau mwingine.

Nao washiriki toka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza wamesisitizwa kuzingatia mafunzo yaliyotolewa na kuyatumia vyema ili kujenga uwezo kwa kamati zao kukabili kwa mafanikio maafa yanapojitokeza sehemu walizopo.

Wakuu na mazungumzo ya hapana pale...

Picha ya pamoja ya viongozi na washiriki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.