ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 3, 2013

TANROAD YACHOMA MABANDA YA WAFANYABIASHARA WAKAIDI MWANZA

TANROAD mkoa wa Mwanza inaendesha zoezi la kuwaondosha wafanyabiashara ndogondogo waliokiuka utaratibu uliowekwa wa kuwataka kutofanya biashara zao kandokando mwa barabara za Mwanza - Musoma na Mwanza - Shinyanga hivi ndivyo zoezi hilo lilivyofanyika huku ulinzi mkali ukihusishwa. 

Kuvamia kwa wafanyabiashara katika maeneo haya ya miliki ya barabara kunasababisha ajali, kuwepo na ufinyu wa watumiaji wa barabara wakiwemo watembea kwa miguu.

Kutokana na kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha mkoa wa Mwanza kilichokaa na kukubaliana na ombi la TANROAD la kuwaondoa wafanyabiashara hao waliojikita ndani ya hifadhi ya barabara.

Gari la TANROAD na vifaa vyake kikazi zaidi.

Zoezi hilo linafanywa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi.

Tokea mwezi wa nne mwaka huu (2013) amri  na muda maalum uliwekwa kwa wafanyabiashara wote waliovamia hifadhi za barabara hizo kuondoka mara moja hivyo zoezi la sasa linawahusu wale waliokaidi. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.