MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.Mabao ya Yanga SC yamefungwa na viungo Mudathir Yahya Abbas mawili dakika ya nane na 34 na Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 67.
Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 44 katika mchezo wa 18 kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tisa zaidi ya watani wao, Simba SC ambao pia wana mechi mbili mkononi.
Kwa upande wao, Pamba Jiji FC baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 26 za mechi 18 sasa wakishuka kwa nafasi moja hadi ya sita.
Tupe maoni yako
.jpeg)
.jpeg)
0 comments:
Post a Comment