NA VICTOR MASANGU/PWANI - SAUTI NA FLORENCIA PETER
Katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ya kuboresha sekta ya elimu wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Sf Group wameamua kuungana kwa pamoja kuitumia siku ya maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani kufanya matendo mbali mbali huruma ikiwemo kutoa msaada wa kompyuta, madaftari, na taulo za kike katika shule ya Koka sekondari na kutembelea vituo vya watoto yatima katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.
Akizungumza katika sherehe za maadhimisho hayo ambayo yamefanyika katika Jimbo la Kibaha mjini Mkurugenzi wa Rasirimali watu na utawala wa kampuni ya SF Group Marygoreth Faustinen amebainisha kwamba wameamua kuitumia siku hiyo katika kutoa misaada mbali mbali ikiwa ni njia moja wapo ya kurudisha fadhila kwa jamii ambayo inawazunguka sambamba na kusaidia kutatua changamoto za wananchi katika baadhi ya maeneo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment