NEW DELHI-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe amekutana kwa mazungumzo na Wawakilishi wa Heshima wa Tanzania katika maeneo ya Nepal, Mumbai, Chennai na Kolkata ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini India.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika jijini New Delhi hivi karibuni wamejadili umuhimu wa wawakilishi hao kushirikiana na Serikali katika kuimarisha sekta ya utalii, kilimo, elimu na biashara na uwekezaji ili kutekeleza dhana ya Diplomasia ya Uchumi.Akizungumza, kwenye kikao kilichofanyika jijini New Delhi hivi karibuni, Mhe. Dkt. Maghembe aliwapongeza wawakilishi hao kwa kuiwakilisha Tanzania kikamilifu kwenye maeneo yao na kwamba Serikali inathamini mchango wao kwenye uwakilishi huo na itaendelea kushirikiana nao.
Kwa upande wao, wawakilishi hao Mhe. Rajesh Chaudhary wa Nepal, Mhe. Nayan Patel wa Mumbai, Mhe. Krishna Pimple wa Chennai na Mhe. Pradeep Singhania wa Kolkata wamemshukuru Mhe. Naibu Waziri kwa kukutenga muda wa kukutana nao na kwamba wataendelea kuiwakilisha Tanzania kikamilifu kwenye maeneo yao hususan katika kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini ikiwemo utalii biashara na uwekezaji.
Mhe. Maghembe ambaye yupo nchini India kwa ziara ya kikazi pamoja na kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Raisina, kwenye kikao hicho aliongozana na Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Anisa Mbega na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Felista Rugambwa.Tupe maoni yako












0 comments:
Post a Comment