ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 25, 2026

NI RASMI SASA MO SALAH ATAONDOKA RASMI LIVERPOOL

  Mohamed Salah poses with the Premier League trophy

Mohamed Salah ataondoka Liverpool msimu huu akiwa miongoni mwa wachezaji bora kabisa kuwakilisha klabu hiyo na kung'ara katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL)


Takwimu za Salah zinaonyesha mafanikio yake kwa uwazi, lakini zaidi ya hiyo, kuna hadithi kubwa nyuma ya namba hizo. Mashabiki zake pale Anfield, ambao wanamuita 'Egyptian King' (Mfalme wa Misri), wanakumbuka kila goli lake alilofunga na kila mchango wake kwenye klabu hiyo, jambo ambalo limeifanya historia yake kuwa ya kipekee.

Salah alijiunga na Liverpool kutoka AS Roma mnamo Juni 23, 2017 kwa ada ya pauni milioni 34, kiasi kinachoonekana sasa kama fedha ndogo ikilinganishwa na mafanikio aliyoyapata baada ya kuhamia Liverpool.


Kama Kevin de Bruyne, Salah alikuwa Chelsea awali lakini hakufanya alichotarajiwa, akifunga mabao mawili tu katika mechi 19, akianza katika michezo 10 tu.

Awali aliikataa Liverpool pale alipoondoka Basel na kujiunga na Chelsea Januari 2014. Kumbukumbu yake ya kwanza Anfield ilikuwa pale alipoanza kwenye jezi ya Chelsea katika ushindi wa 2-0 mnamo Aprili 2014, mchezo unaokumbukwa kwa kosa la Steven Gerrard kosa lililozima ndoto za ubingwa uliokwenda Manchester City.

Hata hivyo, tangu alipojiunga rasmi na Liverpool, Salah ameacha kumbukumbu zisizosahaulika, akisaidia klabu hiyo kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya, mataji mawili ya Ligi Kuu, Kombe la FA, EFL Cup sasa Kombe la Carabao, UEFA Super Cup na Kombe la dunia la vilabu, akiboresha historia ya Anfield.


Safari ya maana ya Salah kutoka Basel mpaka Liverpool

Salah alianza safari yake yake polepole Basel, ambapo kocha Murat Yakin aligusia kwamba atakuwa mchezaji nyota pale alipoifunga Tottenham katika robo fainali ya Europa League 2013.


"Kama Mohamed ataendelea kufunga mabao zaidi, hatasalia hapa," Yakin alisema. Na kweli hakusalia, akaendelea kuwa kwenye kiwango bora. Baada ya kuondoka Chelsea, baadaye kwa mkopo Fiorentina kisha AS Roma, Salah alijitengenezea jina kubwa kabla ya kuwasili Anfield, na hata Klopp huenda hakuwa amejua anamchukua mtu wa mwenye kiwango gani hasa.


Goli lake la kwanza akiwa na Liverpool lilikuwa katika sare ya 3-3 dhidi ya Watford. Tangu hapo, hakukoma kufunga. Salah ameifungia Liverpool jumla ya mabao 255 katika mechi 435, akishika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji bora wa klabu hiyo, nyuma ya Ian Rush na Roger Hunt. Katika Ligi Kuu, amecheza mechi 310, akifunga mabao 189 na kutoa pasi za mabao 92, akichangia jumla ya mabao 281, mchango mkubwa zaidi kwa klabu moja katika historia ya Ligi Kuu.


Salah alikuwa mchezaji mwenye ubinafsi wa kipekee lakini pia alichangia kikamilifu kwa timu. Msimu wake wa kwanza ulikuwa mzuri sana, akifunga mabao 44 na kutoa pasi 14 katika mechi 52. Hata hivyo, aliumia kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid, akicheza dakika 31 tu. Mwaka mmoja baadaye, alirekebisha hilo pale Liverpool iliposhinda 2-0 dhidi ya Tottenham, akifunga penati ya mapema.


Salah alikuwa sehemu ya safu bora ushambuliaji akiwa na Sadio Mane na Roberto Firmino, wakiwa na kasi, mbinu na ufanisi wa timu. Alishambulia kutoka upande wa kulia, Mane upande wa kushoto, na Firmino akibadilisha nafasi akicheza kama shambuliaji ama nyuma ya mshambuliaji, ambaye ufundi wake ulisaidia kuboresha viwango vya kila mmoja.


Kila msimu, Salah aliendelea kuwa na uthabiti mkubwa. Katika mechi 310 za Ligi Kuu, kiwango cha ushindi wa Liverpool kilikuwa 63.9%, na katika jumla ya mechi 435, kilikuwa 62.7%. Hii inaonyesha miaka ya heshima kwa klabu na mchezaji.


Hata hivyo mwishoni mwa zama zake hizi, kabla ya michuano ya AFCON, Salah alikabiliana na changamoto ya kocha mpya Arne Slot, baada ya Klopp kuondoka. Kukawa na malumbano kwa sababu ya kuwekwa benchi, lakini mara zote alithibitisha ni bora alipopata nafasi. Baada ya msimu huu wa mwisho, Salah ataondoka akiwa amejenga urithi usioweza kuharibiwa.


Hakuna anayekinzana na ukweli kwamba Mohamed Salah amekuwa miongoni mwa wachezaji bora kabisa kuwahi kuvaa jezi nyekundu ya Liverpool.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment