ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 25, 2026

MWAKILISHI JIMBO LA CHWAKA AWAKOMBOA WANAFUNZI KWA KUTOA MSAADA WA VIFAA VYA ELIMU

 


NA MWANDISHI WETU, CHWAKA

 
Katika kuboresha sekta ya elimu  Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka Mhe. Issa Gavu leo machi 25 amekabidhi vitabu kwa ajili ya kujisomea pamoja na vifaa mbali mbali vya elimu lengo ikiw ni kuleta mabadiliko katika suala zima la kukuza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa skuli  zote la Jimbo hilo.

Akikabidhi msaada huo Mwakilishi wa Jimbo hilo la Chwaka Mhe Gavu amebainisha kwamba wameamua kutoa msaada wa vifaaa mbali mbali kwa wanafunzi hao ikiwemo kompyuta mapakato,Printer, vitabu m,bali mbalin pamoja na mashine ya kubuluzia karatasi (Photocopy mashine)  vyote vikiwa vimegharimu kiasi cha shilingi milioni 12 msaada ambao umetolewa kutoka kwa marafiki wema kwa watu wa Jimbo la Chwaka.


"Leo tumejumuika hapa kwa ajili ya kuweza kukabidhi vifaa mbali mbali kwa wanafunzi ambao wanasoma katika Jimbo la Chwaka na katika siku ya leo tumeweza kukabidhi vifaa mbali mbali ikiwemo vitabu kwa ajili ya kujisomea wanafunzi, Photocopy mashine, pamoja Printer ambavyo vitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wanafunzi kuweza kuongeza kasi ya ufaulu katika masomo yao,"amebainisha Mhe. Gavu.

 Aidha katika tukio hilo pia Mhe. Gavu kwa kushirukiana na marafiki zake wa Jimbo hilo pia wameweza kutoa msaada wa  kugawa  mabati katiika  Skuli ya Mrembo Uroa, washing machine, tanki  la maji na mipira Jendele, pamoja na mafeni na vifaa vya umeme kwa Kituo cha Afya Cheju.


Mhe  amesema  kwamba wameamua kutoa misaada hiyo katika nyanja mbali mbali ikiwa ni moja ya hatua ya kuweza  kuimarisha suala la  elimu kwa wanafunzi  pamoja na kuboresha afya kwa jamii ambayo inawazunguka hasa katika Jimbo la Chwaka na kuwasihi wanafunzi waweze kusoma kwa bidii lengo ikiwa ni kupata na kuongeza maharifa  ambayo yatawasaidia katika siku za usoni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment