ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 10, 2026

MAAFA YA MVUA YAFUNGA MTAA MKUYUNI, WAFANYABIASHARA WASAFIRI WAHAHA.

 🚨𝗠𝗸𝘂𝘆𝘂𝗻𝗶: 𝗠𝗮𝗮𝗳𝗮 𝘆𝗮 𝗺𝘃𝘂𝗮 𝘆𝗮𝗺𝗳𝘂𝗻𝗴𝗮 𝗺𝘁𝗮𝗮, 𝘄𝗮𝗳𝗮𝗻𝘆𝗮𝗯𝗶𝗮𝘀𝗵𝗮𝗿𝗮 𝘄𝗮𝗸𝗮𝘁𝗮 '𝗛𝗮𝘁𝘂𝗺𝘄𝗶 𝗺𝘁𝗼𝘁𝗼 𝗱𝘂𝗸𝗮𝗻𝗶'

.
Majira ya asubuhi ya leo tarehe 10/03/2026 eneo la Mkuyuni lilishuhudia mafuriko makubwa baada ya mvua kuendelea kunyesha, hali iliyofanya barabara zisipitike na maji kujaa kwa kiwango kinachoharibu biashara na maduka kandokando ya barabara.
.
Mvua ilianza mdogomdogo mapema alfajiri na kuongezeka kuanzia saa 2:30 hadi 4:00 asubuhi, ikichapa ile yenyewe, ikisababisha wateja kukosa uwezo wa kufika sokoni na wafanyabiashara kulazimika kufunga maduka.
.
“Maji yalikuja ghafla na kujaa dukani nikalazimika kupandisha juu bidhaa zote nilizokuwa nimeziweka chini sakafuni — hatumwi mtoto dukani,” alisema mfanyabiashara mmoja wa sokoni, akieleza wasiwasi wa wafanyabiashara waliokuwa wameweka bidhaa mafuta za mauzo.
.
Hadi sasa mamlaka za mkoa au wilaya hazijatoa taarifa rasmi kuhusu uzito wa uharibifu au idadi ya wahasiriwa.
.
#jembehabari
#DriveMix

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment