ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 13, 2026

DARAJA LA RUHEMBE LAKATIKA SAFARI ZASIMAMA

Daraja la Ruhembe. Wananchi wanaotumia barabara ya Mikumi kuelekea Ifakara, Ulanga, Mlimba na Malinyi wamelazimika kusitisha kwa mara nyingine safari baada ya Daraja la Ruhembe lililopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro kuharibika kwa kukatika kingo zake.

Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 13 na kusababisha magari pamoja na vyombo vingine vya usafiri kushindwa kupita katika eneo hilo.

Barabara hiyo ni kiungo muhimu kwa wakazi wa wilaya za Kilosa, Kilombero, Ulanga pamoja na Malinyi ambao hutegemea njia hiyo kusafirisha abiria na bidhaa mbalimbali.
Kutokana na hali hiyo, wananchi wamelazimika kusubiri hatua za dharura huku baadhi yao wakitumia njia mbadala kufikia maeneo yao.

Awali daraja jingine katika barabara hiyo eneo la Kijiji cha Mhenda lilikatika  Kingo zake usiku wa kuamkia Machi 09 mwaka huu ambapo Uongozi wa Mkoa wa Morogoro uliwataka wataalamu wa wakala wa barabara TANROADS kuchukua hatua za haraka kujenga kivuko cha muda ili kurahisisha wananchi kuvuka kwa miguu wakati jitihada za kurekebisha daraja la kudumu zikiendelea.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment