ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 12, 2026

TATHIMINI YA ZOEZI LA UHAMAJI WA HIARI WA WAKAZI WA ENEO LA HIFADHI YA NGORONGORO

 

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka akizungumza katika hafla ya kupokea Taarifa za Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma, tarehe 12 Machi, 2026.

Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Katibu Mkuu Mstaafu, Mhandisi Musa Iyombe akizungumza na kukabidhi Taarifa ya Tume hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma, tarehe 12 Machi, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye hafla ya kupokea Taarifa za Tume ya Rais ya Kutathmini Mgogoro wa Ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Tume ya Rais ya Kutathmini Zoezi la Uhamaji wa Hiari wa Wakazi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 12 Machi, 2026.

Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kutathmini Masuala ya Ardhi katika Wilaya ya Ngorongoro, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Dkt. Gerald Ndika akizungumza na kukabidhi Taarifa ya Tume hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma, tarehe 12 Machi, 2026.
Rais Dk Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi katika utekelezaji wa mapendekezo ya Tume za Rais kuhusu mgogoro wa ardhi na uhamaji wa hiari Ngorongoro kwa maslahi yao na nchi kwa ujumla.

Samia ametoa kauli hiyo, leo Alhamisi Machi 12, 2026, wakati wa hotuba yake, katika hafla ya kupokea taarifa ya Tume za Rais kuhusu mgogoro wa ardhi na uhamaji wa hiari, Ngorongoro.

“Tumesikia kwamba Serikali tulifanya kwa nia njema lakini tulikosea baadhi ya maeneo na hayo ndio ya kukaa kutafakari na kuona namna ya kurekebisha,” amesema.

Amesema ni matumaini yake mapendekezo yaliyomo ndani ya taarifa hiyo, yataiongoza Serikali kupata namna bora ya kushughulikia jambo hilo kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Ameitaka Ofisi ya Waziri Mkuu isimamie utekelezaji wa mapendekezo hayo na yaratibiwe kwa kushirikiana na Katibu Mkuu Kiongozi.

Amesema anatambua mchakato wa utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na tume unaweza kuibua mitazamo tofauti katika jamii hasa kutoka kwa wale wanaofaidika.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment