ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 8, 2026

CHAMA NA LOEMBA WAFUNGA SIMBA SC YASONGA MBELE KOMBE LA CRDB

 


VIGOGO, Simba SC wamejikatia tiketi ya Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya B19 usiku wa jana Jumamosi katika Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na viungo, Mkongo-Brazzaville, Inno Jospin Loemba dakika ya 22 na Mzambia, Clatous Chotta Chama dakikia ya 77.

Mechi nyingine za Hatua ya 32 Bora Kombe la CRDB leo timu ya Namungo FC imefanikiwa kutinga 16 Bora baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya kagera Sugar jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Nyota wa mchezo huo ni kiungo, Jacob Raymond Massawe aliyefunga mabao matatu peke yake dakika ya 11, 28 na 45, huku bao lingine likifungwa na winga Hassan Salum Kabunda dakika ya 89 baada ya Kagera Sugar kutangulia na bao la Hamisi Adam dakika ya nane. 

Nayo Pamba Jiji FC imesonga mbele kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Transit Camp ya Dar es Salaam jioni ya Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, wakati Geita Gold imeichapa Nyika ya Pwani 4-1 Uwanja wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu mjini Geita na Mashujaa FC imeitoa KegGold ya Mbeya kwa penalti 5-3 baada ya sare ya bila mabao ndani ya dakika 90 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment