MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cosmopolitan katika mchezo wa Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) usiku wa jana 18 February 2026 Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao yote ya Yanga leo yamefungwa na mchezaji mpya, winga Mgambia, Buba Jammeh aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka Interclube ya Angola dakika ya 13 na 23 ya mchezo huo wa Hatua ya Timu 64.
Yanga sasa wanasonga mbele ya Raundi ya Tatu ya michuano hiyo itakayohusisha timu 32 katika kampeni ya kutwaa taji la michuano hiyo kwa Mara ya tano mfululizo.
Tupe maoni yako

0 comments:
Post a Comment