ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 12, 2026

KUMEKUCHA DODOMA, TBN IPO TAYARI KWA UFUNGUZI WA ABC 2026!

 


Kutoka katikati ya mji mkuu wa Serikali, Dodoma,  Februari 12, 2026, tasnia ya habari itakutana katika ukumbi wa New Generation kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji (ABC).


Mgeni Rasmi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda, atazindua rasmi mkutano huu ambapo TBN pia itatoa salamu zake za mwanzo.Mwenyekiti ataongoza wanablogu 60 wanachama wa TBN kusikiliza waziri na kutoa mmichango yaouendelezaji wa sekta.

Nini kipo mezani kesho kutokea TBN?

Sauti ya Wanablogu 200+: TBN itatoa salamu za wadau, ikisimama kama "Balozi wa Kidijitali" anayepambania amani, utulivu, na maendeleo ya nchi yetu.

Kurekebisha Algorithim za AI: TBN itaelezea mpango wake wa kizalendo wa kurekebisha taswira ya Tanzania mtandaoni kwa kushibisha anga la kidijitali na maudhui bora ya ndani ili kuondoa "madudu" ya AI.

Shukrani kwa Serikali na TCRA: Tutatumia jukwaa hili kuishukuru serikali kwa kusikia kilio chetu na kuanza mchakato wa kupunguza vizingiti vya ada na leseni, jambo linalochochea ajira kwa vijana.

Uzalendo wa Kidijitali: Task force yetu inaendelea kufanya kazi kuhakikisha Tanzania inang'ara kimataifa katika uwekezaji na utalii kupitia habari chanya.

Tukutane ukumbi wa New Generation au fuatilia kurasa zetu kwa updates za dakika baada ya dakika!

#ABC2026 #TBNDodoma #PaulMakonda #TCRA #NewGeneration #DigitalTanzania #AmaniNaMaendeleo #MabaloziWaKidijitali

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment