ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 21, 2024

KAGERA SUGAR YAPATA MNYONGE, YAICHAPA KEN GOLD 2-0 KAITABA


IJUMAA 20 SEPT 2024 
WENYEJI, Kagera Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ken Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na mshambuliaji Mganda, Peter Lwasa dakika ya kwanza na 65 na ushindi huo wa kwanza unaifanya timu hiyo ifikishe pointi nne katika mchezo wa tano kufuatia kufungwa mechi tatu awali na kutoa sare moja.

Kwa upande wao Ken Gold waliopanda Ligi Kuu msimu huu wanafikisha mechi nne bila ushindi, tena wakifungwa zote 3-1 na Singida  Black Stars, 2-1 na Fountain Gate na 1-0 na KMC.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.