NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mke wa Mbunge wa jimbo la Kibaha Mama Selina Koka kwa kushirikiana na wanawake wa kata ya Tumbi wamefanya kongamano maalumu kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Katika kongamano hilo ambalo limehudhuliwa na mamia ya wanawake kutoka kata ya Tumbi na maeneo mengine ya Jimbo la Kibaha mjini pamoja na viongozi wa serikali,viongozi wa chama ikiwa pamoja na baadhi ya Wabunge.
Akizungumza katika kongamano hilo Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka amesema lengo kubwa ni kuwahimiza ushiriki wa Wanawake katika chaguzi zijazo ikiwemo Serikali za Mitaa.
Mama Koka ambaye pia ni Mlezi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini amebainisha kuwa kongamano hilo ni kwa ajili ya kuwatia moyo wanawake kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbali mbali za uongozi bila uwoga wowote katika chaguzi mbi mbali.
"Mimi kama mke wa Mbunge kwa kushirikiana na wanawake wa kata ya Tumbi pamoja na maeneo mengine tumeona umuhimu wa kukutana kwa pamoja na kujadili mambo mbali mbali hasa katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mtaa,"alisema Mama Koka.
Aidha Mama Koka aliongeza kuwa katika kongamano hilo limekwenda sambamba na mafunzo kutoka taasisi za fedha juu ya ujasiriamali na utunzaji wa fedha na fursa za miķopo zilizopo.
Aidha Mama Koka alisema kongamano hilo litakuwa likifanyika kila mwezi Septemba kwa lengo la kuwakutanisha wanawake katika kata zote 14 za Jimbo la Kibaha ili kujadili mambo mbali mbali ya kimaendeleo na changamoto zinaziwakabili.
Akizungumza na Wanawake walioshiriki kongamano hilo kutoka maeneo mbalimbali ya Mji wa Kibaha Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Zainabu Vullu amesema wanatakiwa kuhamasishana kugombea nafasi za uongozi.
Amesema kwa kufanya hivyo itasaidia kuongeza viongozi Wanawake kwenye mitaa yetu na Vijiji katika uchaguzi unatarajia kufanyika Novemba mwaka huu.
Vullu pia amewakumbusha wananchi kuchagua viongozi bora sio bora kiongozi ambao watawasaidia kuvuka kwenye mapambano ya kiuchumi.
"Tukachague viongozi bora kwasababu ndio tunaweka misingi ya mitano tena kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan hayo ndio malipo yetu kwa Rais amefanya mambo mengi ambayo ni neema kwa wananchi, amemtua mama ndio kichwani na mengine mengi kwenye Jamii," amesema.
Pia amepongeza Mlezi wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Kibaha mjini kwa kushiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii huku akimuomba kusaidia kuandaa andiko la mradi litakaloenda kwenye Taasisi za fedha ambalo litakalokuwa msaada na Wilaya nyingine katika kuwakwamua Wanawake kiuchumi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amewapongeza wanawake wa kata ya Tumbi pamoja na mkewe kwa kuandaa kongamano hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.