ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 20, 2024

KOKA ATUMIA MFUKO WA JIMBO KUBORESHA SEKTA YA ELIMU KATA YA TANGINI

 


NA VICTOR MASANGU,KIBAHA


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu ameahidi kutumia fedha za mfuko wa jimbo kwa asilimia 85 kwa ajili ya kuboresha elimu.

Koka ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya  kikazi kwa ajili ya kuweza kutembelea na kugagua miradi mbali mbali ya maendeleo katika kata ya Tangini.

Koka amesema kwamba lengo lake kubwa ni kuweka mikakati kabambe ambayo itaweza kusaidia kuboresha elimu katika maeneo mbali mbali ikiwemo kuboresha miundombinu ya majengo madarasa pamoja madawati.

Aidha Koka amebainisha katika ameweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 11.5 kwa lengo la kuboresha miundombinu ya madarasa ambayo yalikuwa maboma katika shule ya msingi Mamlaka.
Pia amebainisha kwamba ameweza kuchangia jumla ya madawati yapatayo 100 katika shule hiyo ya msingi Mamlaka.

Pia Mbunge Koka amempongeza kwa dhati Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutenga kiasi cha zaidi ya milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari kata ya Tangini pamoja na ujenzi wa mradi wa ujenzi wa Zahanati.


Alibainisha kwamba katika miradi ya ujenzi wa shule mpya  ya sekondari na zahanati ya mtaa wa kilimahewa itaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wanafunzi na wananchi.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mamlaka Rucy Nzutu amemshukuru Mbunge Koka kwa juhudi zake za kukuza na kusaidia sekta ya elimu kwa vitendo.

Naye Diwani wa Kata ya Tangini Mfaume Kalanguti amesema wananchi walikuwa wanakabiliwa ukosefu wa huduma ya shule ya sekondari pamoja na zahanati. 

Nao baadhi ya wananchi wa  Kata ya Tangini wamemshukuru Rais Samia pamoja na Mbunge kwa kuweza kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa vitendo.

Ziara ya  kikazi ya  Mhe.Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini katika Kata ya Tangini imeweza kutembelea shule ya msingi Mamlaka,mradi wa ujenzi wa zahanati na ujenzi wa shule mpya ya sekondari pamoja na kuzungumza na wananchi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.