UONGOZI
wa Klabu ya Simba Sc, umeweka wazi kuwa kwenye anga la kimataifa katika Kombe la Shirikisho
Afrika hawataki kuishia hatua ya pili bali malengo ni kuona kwamba wanatinga
hatua ya makundi.
Kazi
pekee inayohitajika kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids ni kupata
ushindi kwenye mchezo ujao dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya unaotarajiwa
kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 22 baada ya mchezo wa awali kusoma 0-0.
Ahmed
Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa mpango mkubwa
uliopo kwa timu hiyo ni kusaka ushindi kwenye mchezo wao ujao na wanatambua
inawezekana hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.
“Wote mliona vijana wetu waliocheza kwa nidhamu pale Libya licha ya vurugu zote. Sasa ngoma inahamia nyumbani twendeni tukawape nguvu vijana wetu wakatupeleke hatua ya makundi"
"Jambo la kushinda ni la kila Mwanasimba. Mechi yetu ndio yenye mvuto zaidi Afrika wikiendi hii. Na sisi kama Mnyama hatutaki kuishia hatua hii kwa mapenzi yake Mwenyezi Mungu. Tunayo timu nzuri sana, tuna kikosi kizuri sana lakini pia viongozi wenu tumejipanga kuhakikisha Simba yetu inafuzu makundi."
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.