Kulingana na askofu huyo ni
kuwa alielezwa na Mungu kuwa angelipata fuvu la kichwa ya mwanadamu katika ufuo
wa Ziwa.
Ododo anasemekana kuwaeleza
wafuasi wake mkesha wa usiku wa pasaka kuwa alikuwa amepata maono kutoka kwa
Mungu kuwa angepata fuvu la kichwa cha binadamu ndani ya maji.
Taarifa ya polisi imeeleza kuwa Ododo alikuwa amepata mwaliko
kuhubiri katika kanisa lililoko eneo la
Gembe Magharibi siku ya Jumamosi na kuwa wakati wa maombi katika kanisa hilo
ndipo Askofu huyo alidai kupokea maono kutoka kwa Mungu.
Wafuasi wa Ododo
wanasemekana kumuamini askofu huyo na kumfuata katika fuo la Ziwa ambako
walipata fuvu la kichwa cha mwanadamu na kisha wakaiteketeza.
Kulingana na Naibu Chifu wa
Lokesheni Ndogo ya Kasgunga Mashariki Francis Kasuku suala hilo lilijulikana
baada ya wakazi kuanza kusambaza habari hizo kwenye mitandao ya kijamii.
Kasuku anasemekana kuripoti
kisa hicho kwa maafisa wa polisi ambao aliwataka wamhoji askofu huyo na wafuasi
wake kuhusu hatua yao ya kuchoma fuvu la kichwa cha mwanadamu.
Imesemekana kuwa polisi
walipofika kumhoji mshukiwa tayari alikuwa ashatoweka na kuwa wafuasi wake
waliohojiwa walisema kuwa ni yeye alikuwa mhusika mkuu katika tukio hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.