Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justine Nyamoga akiwa amepanda usafiri wa boda boda na kusema kuwa usafiri wa boda boda ni usafiri mzuri kama ulivyo usafiri mwingine.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justine Nyamoga akiwa amepanda usafiri wa boda boda na kusema kuwa usafiri wa boda boda ni usafiri mzuri kama ulivyo usafiri mwingine
Na Fredy Mgunda, Kilolo.
MBUNGE wa Jimbo la Kilolo, Justine Nyamoga amesema bodaboda ni ajira na kazi kama zilivyo nyingine.
Nyamoga amesema hayo baada ya kupanda usafiri huo wakati akielekea kushiriki michuano ya Justine Nyamoga Easter Cup iliyofanyika Ilula, Wilayani Kilolo.
"Nimepanda bodaboda kwa sababu huu ni usafiri na hii ni ajira kama zilivyo ajira nyingine," amesema Nyamoga na kuongeza;
"Wapo wanaoendesha bodaboda na baadae wanastaafu wakiwa wazima. Wapo ambao bahati mbaya wanakumbana na changamoto kama ilivyo kwenye kazi nyingine. Kila kazi inachangamoto na uzuri," amesema Nyamoga.
Mbunge huyo amefanikiwa kuendesha michuano ya Nyamoga Easter Cup akikutanisha timu nane za mpira wa miguu na bao.
Pia amekabidhi jezi kwa kila timu huku akitoa zawadi kwa mshindi wa kwanza, pili na watatu kwa timu za mpira wa miguu.
Kwa mchezo wa bao, Mbunge ametoa zawadi kwa mshindi wa pili na wakwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.